UNASEMAJE UMEOKOKA?
UNASEMAJE UMEOKOKA ❓
🔹Unasemaje umeokoka wakati unavaa vinguo vya ajabu ajabu, visketi vifupi hata kuinama hauwezi na bado vina mpasua, visuruali vinakubana mpaka maumbile ya ndani yanaonekana.
👉Wewe utakuwa una roho ya kikahaba inakusumbua sio Bure.
🔹Unasemaje umeokoka wakati una shinda na walevi, wazinzi, waongo na watu wasiofaa bila hata kuwaambia KWELI ya MUNGU kuwa waache dhambi zao? Na badala yake unafurahi nao pamoja kama vile hamna shida.
👉Ndugu damu ya hao watu itadaiwa mikononi mwako.
🔹Unasemaje umeokoka wakati simu yako imejaa movies Za ngono (ponography), manyimbo ya bongofleva, msondo ngoma, taarabu na mapicha ya utupu?
👉Mungu hachanganywi, chagua moja kuifuata dunia na uhukumiwe au kumfuata Mungu uikoe Nafsi yako. Huwezi kutumikia mabwana wawili. Huo nao ni Ukahaba /uzinzi wa Kiroho. Yakobo 4 :4-10
🔹Unasemaje umeokoka wakati mwaka mzima unaisha haujafunga hata siku moja na biblia haujasoma zaidi ya kuifungua jumapili kanisani huku upo Full online Facebook, Watsap na mitandao mingine ya kijamii?
👉Badilika saa usiyodhani Mwana wa Adamu atarudi kulichukua kanisa Lake.
🔹Unasemaje umeokoka wakati ni mzinzi, muongo, mchonganishi na umetoa mimba SI chini ya 3 huku ni kiongozi wa vijna na mwana praise kanisani
.
👉Mungu HADHIHAKIWI kile unachopanda ndicho UTAKACHOVUNA. Galatia 6 :7-8
🔹Unasemaje umeokoka wakati hapo ulipo una wachumba zaidi ya 5 na wote umewaahidi kuwaoa?
👉Usipotubu upesi, roho ya mauti ipo njian kukumaliza.
🔹Unasemaje umeokoka wakati majirani zako, wapangaji wenzako na hata nyumbani kwako hata amani hakuna na wewe ndio chanzo cha yote hayo? Ukifika kazini hata kama watu walikuwa wanacheka ghafla watakunja ndita kwa tabia zako zisizofaa.
👉Ukristo ni maisha matakatifu na matendo mema na si kwenda kanisani peke yake. Pia ibada njema huanzia nyumbani. Ishi kwa ushuhuda Mwema.
🔹Unasemaje umeokoka wakati una hama hama makanisa kama vyama vya siasa? Leo upo kwa mzee...... Ubungo, kesho upo mwenge, kesho kutwa Temeke.
👉Ndugu hiyo ni roho ya kutanga tanga inakusumbua. Wewe ni sawa na Mkimbizi wa Kiroho. Jirekebishe.
🔹Unasemaje umeokoka na tena unajiita mtumishi wakati ni mlevi, mzinzi na tapeli? Unatumia utumishi kama mwamvuli wa kujikingia Uovo wako.
👉Adhabu yako itakuwa kubwa zaidi hata ya wale ambao hawajamjua Mungu. Mathayo 7 :22-23
"BASI KUMBUKA NI WAPI ULIKOANGUKA UKATUBU, UKAYAFANYE MATENDO YA KWANZA.
'LAKINI USIPOFANYA HIVYO, NAJA KWAKO, NAMI NITAKIONDOA KINARA CHAKO KATIKA MAHALI PAKE. USIPOTUBU "
UFUNUO 2 : 5.
YESU YU KARIBU KUJA.....KAA TAYARI
0 comments:
Post a Comment