KWANINI MWANAMKE USIVAE SURUALI..!
🔹Kumekuwa na mada nyingi na maswali mengi kuhusu mabinti
kuvaa suruali (hasa waliookoka), michango mingi na mafundisho mengi yametolewa,
nami naomba niongezee kitu kidogo.
🔹Zifuatazo ni sababu kwanin binti hautakiwi kuvaa suruali...
👉HAISITIRI MWILI.!
🔹Neno la Mungu linaagiza wanawake wavae Mavazi yanayositiri
(yanayofunika /yanayoficha Mwili) 1 Timotheo 2 :9
🔹Lakini vazi la suruali kwa mabinti halisitiri Mwili na
badala yake yanauonesha /yanautangaza mwili uonekane vizuri. Hivyo hukiuka
agizo la Mungu.
🔹Mwili wa mwanamke ni wa thamani sana na haupaswi kuonekana
ovyo hasa sehemu kama matiti, kiuno, kitovu na mapaja. Ingawa suruali inaweza
isioneshe sehemu hizo lakini bado inauchonga mwili wa mwanamke na kuufanya
usiwe siri tena bali uwe wazi.
🔹Vazi la suruali kwa mwanamke lilibuniwa ili kufanya umbile
(shape) ya mwanamke lionekane vizuri na kuongeza mvuto /uzuri wa mwanamke, na
wakasahau jukumu kubwa na la kwanza la Mavazi ni kuuficha mwili.
👉HUCHOCHEA UZINZI.
🔹Neno la Mungu linasema yeye amtazamaye mwanamke na kumtamani
amekwisha kuzini nae moyoni Mwake, Mathayo 5 :28
🔹Mwanaume kwa asili ni mtu wa tamaa, hii haijalishi awe
anamjua Mungu au la, kinachotofautiana ni uwezo tu wa kujizuia tamaa hiyo.
🔹Ndio maana mtumishi wa Mungu Ayubu aliwejiwekea msimamo kuwa
hatamtazama mwanamke kwa kumtamani (Ayubu 31 :1)
🔹Sasa kwa vazi hilo kwa wanawake pamoja na Mavazi mengine
yasiyositiri mwili yanawakosesha wangapi? Yanawafanya wangapi kuzini kila siku
kwa tamaa ya macho?
🔹Neno la Mungu linasema mtu yeyote atakayemkosesha mwenzake
kufanya dhambi na akamkosa Mungu, basi AFUNGWE JIWE SHINGONI NA ATUPWE
BAHARINI. Dada kama kuna watu unawakosesha na kuwafanya wafanye dhambi HAKIKA
HUKUMU YAKO IPO (Mathayo 18 :6-7).
👉SIO UTAMADUNI WETU WAKIAFRIKA NA KINYUME NA NENO LA MUNGU.
🔹Utamaduni ni wa muhimu sana kuzingatiwa tunapojadili kuhusu
swala la Mavazi. Hata biblia huheshimu tamaduni Za watu isipokuwa zile ambazo
zipo kinyume na Neno la Mungu.
🔹Kwa Utamaduni wetu wa kiafrika hauruhusu mwanamke kuvaa
suruali, mambo ya kuvaa suruali yamekuja miaka ya hivi karibuni kutokana na
utandawazi na watu kuanza kuiga tamaduni Za kigeni (wazungu).
🔹Neno la Mungu linasema mwanamke asivae Mavazi yampasayo
mwanaume na mwanaume asivae Mavazi yampasayo mwanamke, na yeye afanyaye hivyo
ni CHUKIZO kwa BWANA (Kumbukumbu 22 : 5)
🔹Kutokana na Utamaduni wetu ninaweza kusema, mwanamke asivae
Suruali (vazi limpasalo mwanaume) na mwanaume asivae Sketi (vazi limpasalo
mwanamke).
🔹 Ingawa kwa baadhi ya nchi kama Scottish wanaume walikuwa
wanavaa Sketi, ila huo ndio ulikuwa Utamaduni wao sijafahamu kwa Sasa kama
imebadilika.
🔹Utamaduni Inabidi uzingatiwe na si kuamini kila kitu cha
Mzungu kipo sahihi.
# MZUNGU SIO MUNGU.
👉MAVAZI YANABEBA UTAMBULISHO.
🔹Vazi unalovaa linaweza kukutambulisha hata kama
haujajitambulisha. Ukimuona Askari unaweza ukamtambua kutokana na vazi lake
(uniform yake), Ukimuona daktari pia kwenye vazi lake la kazi bila hata
kujitambulisha utamfahamu kama ni daktari. Je, vazi lako la suruali
linakutambulishaje?
🔹Mithali 7 :10, "Na tazama, mwanamke akamkuta, ana
MAVAZI YA KIKAHABA"
🔹Andiko hapo juu 👆linasema mwanamke ana Mavazi
ya kikahaba, Je Mavazi ya kikahaba ni yapi? Nguo yoyote ile isiyositiri mwili
kama Mungu alivyoagiza hiyo ni Nguo ya kikahaba.
🔹Nguo inayokuacha kifua wazi, kitovu, kiuno na mapaja wazi
Nguo hiyo haijauficha mwili hivyo ni vazi la kikahaba. Yapo Mavazi mengi ya
kikahaba na suruali ikiwa ni moja kati ya Mavazi hayo.
🔹Kama tulivyoona mtu aliyevaa vazi la kiaskari ni Askari,
aliyevaa vazi la kidaktari ni daktari, vipi aliyevaa Mavazi ya kikahaba atakuwa
ni nani?
🔹Ni aibu kwa mwanamke anayejiheshimu kuvaa nguo ya kikahaba .
si kila kitu ni cha kuiga,mambo mengine muwaachie wenyewe.
# MAVAZI YA KIKAHABA NI KWA AJILI YA
MAKAHABA, NA SI MWANAMKE ANAYEJIHESHIMU.
👉SURUALI SI VAZI LA HESHIMA KWA MWANAMKE.
🔹Katika Mavazi ya heshima kwa mwanamke suruali si vazi la
heshima. Ingawa wanasema sijui kuna suruali Za kike na kujaribu kuzitetea
Ibilisi ni Ibilisi hata akijifanya malaika wa Nuru.
🔹Kama suruali ni vazi la heshima kwanini wanawake wasilivae
wanapoenda sehemu za heshima mfano msibani? Na hata kama wakivaa basi
watajifunga na khanga juu yake.
🔹Kama suruali ni vazi la heshima kwanin usivae siku unayoenda
kutambulishwa ukweni? Na badala yake unavaa Sketi ndefu mpaka miguuni tena na
khanga juu, lakini cha kushangaza unaenda kanisani na kijisuruali kimekubana
mpaka upindo wa Nguo ya ndani unaonekana, Sketi fupi hata huwezi kukaa kwa
uhuru.
# KAMA UNAHESHIMU UKWENI, SI ZAIDI
NYUMBAN MWA MUNGU ❓
👉MAVAZI UNAYOVAA NI KWA AJILI YA WENGINE.
🔹Mavazi unayovaa si kwa ajili yako ila kwa ajili ya wengine.
Kama Mavazi unayovaa ni kwa ajili yako kwanini usivae ile Nguo yako ya gharama
unayoipenda siku ukiwa hauna ratiba ya kutoka halafu jioni ukaivua? Au siku
utakayoalikwa kwenye sherehe usivae zile yeboyebo zako na ule mtumba wako
ulionunua kwa mmachinga ukaenda nazo?
🔹Nguo nzur au mbaya ni vile watu wanavyoona na si wewe
unavyoona, Nguo hata kama iwe nzur vipi kama watu wanaokuzunguka wakisema
haikupendezi sidhani kama utaivaa.
🔹Suruali na Nguo unayovaa zisizositiri mwili hazikupendezi
ila zina kudhalilisha, na kama mtu anakusifia kama unapendeza huyo hakutakii
mema tena ni kipofu.
🔹Na kipofu akimuongoza kipofu mwenzake wote watatumbukia
kwenye shimo.
........
👉NI WAPI NIVAE SURUALI ❓VAA
SURUALI KAMA KAZI YAKO INAKUBIDI UVAE SURUALI, KAMA UNALALA, UKIWA UNASAFIRI
SAFARI NDEFU ILA UJIFUNGE NA NGUO NYINGINE JUU NA MATUKIO MENGINE
YANAYOKULAZIMU KUFANYA HIVYO.
👉USIVAE SURUALI KAMA FASHION
UKIWA UPO KWENYE MIZUNGUKO YAKO YA KILA SIKU.
"UTII NI BORA KULIKO SADAKA, NA
KUTOKUTII NI SAWA NA DHAMBI YA UCHAWI "
ujumbe mzuri mwalimu; Mungu akuze kipawa chako.
ReplyDeleteAmeen
DeleteMtumishi umeanza vzuri lkn mwisho umeniacha na swali. Umezungumza kwa habari ya uovu wa mwanamke kuvaa suruali. Mwisho umemalizia anaweza kuvaa kulingana na Nazi yake, he so dhambi kuvaa suruali kama unavyoonya? He kuna Mahali ambapo bible inaruhusu kutenda dhambi na kuna wakt tunakatazwa. Mungu ametutofautisha na viumbe vingine vyote. Unao uwezo wa kuchambua mambo. Je wote waliooa hawakuwa na tamaa au walichagua mwanamke tu...? Je km kwa kuvaa suruali mwanamke hajisitiri, kwanini ninyi mnatembea hali hamjavaa nguo? Msiangamie kwa kuyakosa maarifa. Wapi imeandikwa mwanamke atavaa sketi na mwanaume suruali?? Katika biblia nimeona tu ktk mwanzo kuwa Adam na Eva wakajifanyizia mavazi kwa majani. Cyo suali wala sketi. Haya mengine yametokana na sayansi na kukaa kwa technology. Tafakari kwa kina. Mbona basi tusijitengeenezee mavazi kwa majani na tuache kuvaa hizi nguo? ? Kwakuwa tunaenda kinyume na utamaduni wa baba zetu na mama zetu km ilivyo kwa Adam na Eva
ReplyDeleteVzur Kama umetambua tumeumbwa tofaut na wanyama..sisi tumepewa uwepo wa kutofautisha vitu
ReplyDelete