Entertainment


MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KABLA YA NDOA



MADHARA YA KUFANYA MAPENZI (SEX) KABLA YA NDOA..! 

Kuna madhara mengi yanayoweza kujitokeza kwa kuruhusu kufanya mapenzi wakat wa urafiki wa awali au uchumba.

Hapa tutaenda kuangalia baadhi ya madhara hayo.. 

(1). Upendo kupungua au kufa.

Baada ya kufanya mapenz mara nying upendo hupungua hasa kwa vijana wa kiume na kwa mabint upendo huongezeka.
Mabinti wengi wamejikuta wakipoteza THAMANI yao baada ya kuruhusu ku'sex na vijana wa kiume wakidhani kuwa kwa kufanya hivyo upendo utaongezeka kwa mwanaume kumbe wanajitengenezea misiba yao wenyewe.

(2).Mimba.

Hakuna kitu kisichokuwa na malipo. Kile unachopanda ndicho utakachovuna. Ingawa wengi hujaribu kutumia njia za kujizuia wasishike mimba lakini kuteleza kupo. Na wengi hutumia njia hizo wakiwa bado hawajazoena wakija kuzoeana hakuna atakayekumbuka kujizuia tena.

"Ukila tegemea na Kushiba ".


(3).Magonjwa ya Zinaa.

Uaminifu umepungua sana siku hizi na watu kufanya mapenzi tena na watu tofaut imekuwa ni jambo la kawaida. Hali inayoongeza kasi ya maambukizi ya Magonjwa ya Zinaa kama UKIMWI, kaswende, nk.
Si ajabu kumkuta kijana wa miaka 20 ni muathirika wa ugonjwa wa UKIMWI. HALI SI NZURI.

(4).Kukosa Uaminifu baada ya NDOA.

Hii inatokana na hali ya kuzoeana haraka kwa kuanza kufanya Sex kabla ya muda wake. Itafika hatua unajikuta umemzoea mno mwenzako na hakuna kipya usichokijua hivyo utatamani ujaribu radha tofauti.
(5).Kukosa UJASIRI wa kuwafundisha Wanao.

Kama mmejuana kabla ya ndoa, utakuwa na nguvu gani ya kuwaambia Wanao Wajitunze? Utakapoona wanaenda kinyume utaweza kujitolea wewe kama mfano mzuri wa kuigwa ?.

(6).Kubaki na Kovu la KUDUMU.

Kwa kufanya sex kabla ya ndoa, kutakuleta matokeo ya kudumu kama mimba na hatimaye mtoto asiyetarajiwa, Magonjwa kama vile UKIMWI, Kupoteza BIKRA na wengine kuachwa na wapenzi wao baada ya Sex.

Wakat mwingine Kovu linaweza ikawa ni HATIA utakayojisikia Moyoni mwako wakat mwingine hata baada ya KUTUBU.

''Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa, Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
Atapata JERAHA la kuvuniwa heshima,wala FEDHEHA(AIBU) YAKE HAITAFUTIKA"

                  MITHALI 6 : 32-33


(7).KUPOTEZA USHUHUDA.

kufanya Sex nje au kabla ya ndoa ni dhambi. Na kufanya hivyo ni kulitukanisha jina la Yesu aliyekuokoa.

(8).KUKOSEANA HESHIMA BAADA YA NDOA.

Wengi wamejikuta wakiwa katika hali ya kutofautiana mara kwa mara na kujibizana maneno yasiyofaa baada ya ndoa wakati mwanzo hawakuwa hivyo kabla hawajaoana. Wakati mwingine hali hii huwa ni matokeo ya dhambi ya Uzinzi waliyoifanya.

(9).NDOA KUKOSA BARAKA ZA MUNGU.

Hii hutokea wakati watu wapo kwenye uchumba wanafanya dhambi ya Uzinzi kwa SIRI na wanaingia kwenye ndoa bila KUTUBU. Matokeo yake wanajikuta kila wanalofanya haliendi, biashara zinakufa, maelewano hamna, jambo dogo linaweza kuzua ugomvi Usioisha nk. Ukiona mambo kama hayo ujue UTUKUFU WA MUNGU HAUPO.

Ndugu utaweza kuwaficha wanadamu lakini sio Mungu. TUBU MAPEMA.

(10).KIFO cCHA KIROHO.

Dhambi yoyote ile ina mshahara /malipo yake, na matokeo ya dhambi Isiyotubiwa ni kifo cha kiroho (kutengwa na Mungu) na wakat mwingine hata kifo cha kimwili.

"Kwa maana Mshahara wa dhambi ni MAUTI................ " Warumi 6 :23.

*********//****//****/*/**//*////*****

USIKUBALI KUFANYA UZINZI, USIJIRAHISISHE, USISEME NI VIGUMU KUJIZUIA KUFANYA SEX KABLA YA NDOA. NDUGU HAKUNA LISILOWEZEKANA.. NI WEWE KUWEKA MSIMAMO....!

 KUMBUKA HILI...

" MTU AZINIYE NA MWANAMKE HANA AKILI KABISA, AFANYA JAMBO LITAKALOMUANGAMIZA NAFSI YAKE.
'ATAPATA JERAHA NA KUVUNJIWA HESHIMA WALA FEDHEHA (AIBU) YAKE HAITAFUTIKA

 MITHALI 6 :32 - 33.

               SHINDA TAMAA YA MWILI...IKIMBIE ZINAA......DHAMBI INAUA
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.