MASWALI YA KUJIULIZA KABLA YA KUINGIA KWENYE UHUSIANO
MASWALI YA KUJIULIZA KABLA HAUJAANZISHA UHUSIANO NA MTU..!
🔹Yafuatayo ni Maswali ya muhimu kabla haujaanzisha uhusiano na mtu 👇
👉 UNAMFAHAMU VIZURI ❓
NI jambo la Msingi sana kuhakikisha huyo unayetaka kuwa nae unamfahamu vizur. Watu wengi leo huanzisha uhusiano kwa papara bila ya kuwa na ufahamu mzuri na watu hao.
Uhusiano unaanzia kwenye basi, semina, sherehe na kwenye mitandao ya kijamii nk. Msingi wa mahusiano haya mara nyingi ni TAMAA na mwisho wake ni MAUMIVU na MAJUTO kwa mmoja kati yao.
👉UMECHUKUA MUDA GANI KUMTAKIA /KUKUBALI KUWA NAE.
Jipe Muda kabla haujamuambia mtu kama unampenda au kumkubali mtu anapsema anakupenda.
Hii inasaidia nini? Hii itakupa Muda wa kumjua mtu vizur na la muhimu zaidi kufahamu ni kiasi gan amedhamiria kuwa na wewe.
Kuna wengine unawapa Muda wa kusubiri ufikirie zaidi au uombe, unakuta ndani ya mwezi au miezi kadhaa ameshabadili mawazo na kwenda kwa mwingine. Mtu kama huyo ujue alikuwa ni mbabaishaji.
👉UMEKUWA NA WATU WANGAPI NYUMA KABLA YAKE ❓UMEJIFUNZA NINI KATIKA MAHUSIANO YAKO YALIYOPITA ❓
Ni muhimu kujua ni makosa gani uliyofanya au kujifunza katika mahusiano yako ya nyuma, na umejiandaaje ili usirudie hayo makosa.
Bila ya kujiuliza hili, utajikuta unarudia makosa yale yale kwenye huo uhusiano wako unaotaka kuanzisha.
👉JE NI WAKATI SAHIHI KUWA KWENYE UHUSIANO ❓
Kama ni mwanafunzi ni bora ujiepushe na mambo ya mahusiano na ushike lile lililo la muhimu kwa wakat huo. Kama haupo kwenye masomo, basi hakikisha umejiandaa vyema kuingia kwenye uhusiano.
Kukaa Muda mrefu kwenye uhusiano ni mtego wa kuingia kwenye uzinzi, mimba isiyotarajiwa nk.
👉JE UPO TAYARI KUPENDA ❓
Hapa nazungumza na wale ambao wametoka kuumizwa na wenzi wao, ni vizur kujipa Muda wa kusahau machungu na maumivu ya uhusiano uliopita kabla haujaanzisha mahusiano mapya.
Kama bado una kidonda moyon mwako, basi kuna uwezekano mkubwa wa kumuumiza huyo utakayekuwa nae (kwa kuwa moyo wako haujawa tayar kupenda) au kuumizwa tena, na hali yako kuwa mbaya zaidi.
👉UPO TAYARI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZITAKAZOJITOKEZA ❓
Ni vizur ufahamu hakuna uhusiano usio na changamoto na huyo unayeenda kuwa naye si malaika bali ni mtu hivyo ana mapungufu yake.
Usitegemee makubwa saaana kwenye huo uhusiano, mapenzi ni yale yale na watu ni wale wale wametofautiana kwa sehemu lakin jambo la kukumbuka kila mtu ana madhaifu yake.
👉NI NANI MTU WA KARIBU UTAKAYE MSHIRIKISHA KUHUSU UHUSIANO HUO.
Ni vizur kuwa na mtu wa karibu atakayekuwa mshaur wako wa karibu kuhusu uhusiano huo. Kuna mengi utakutana nayo ambayo utahitaji mtu wa kumueleza mambo yako.
Ni vizur Kama akiwa mtu aliye kwenye ndoa unayemuani anaweza kukusaidia. Kwa kuwa ana uzoefu na uelewa mkubwa kukusaidia.
👉UMEPATA MUDA WA KUMUULIZA MUNGU ❓
Uhusiano ulio na uthibitisho wa Mungu, uhakika wa safari ni makubwa kuliko ule unaoanzishwa kibanadamu.
Chukua Muda wa kumuuliza Mungu juu ya huyo unayetaka kuwa nae, huku ukiwa mwaminifu kusubiri jibu lako. Zabur 32 :8
👉NI KITU GANI KITAKACHO KUFANYA UWE NAE ❓
Kama umefuata mambo hayo juu vizur, ni muhimu pia kuwa na sababu ya Msingi inayokufanya uwe naye. Sababu isiwe ni upweke, tamaa ya pesa, hofu ya kuoa au kuolewa nk.
Sababu iwe ni kwa sababu unamfahamu vizur, una uhakika kuwa anakupenda na Mungu amekupa kibali kuwa naye.
..................
🔹MSINGI WAKO NDIO UTAKAOTOA PICHA YA UHUSIANO WAKO UTAKAVYOKUWA.
🔹KAMA MSINGI NI MBOVU USITEGEMEE KUWA NA UHUSIANO /NDOA ILIYO NA USHUHUDA MZURI.
🔹MAAMUZI YAKO NDIYO HATIMA YAKO. ***THINK CAREFULLY & ACT WISELY
👉MARRIAGE IS YOUR DESTINY..!
MWL JOHN C NTOGWISANGU
WATSAP 0712463344
0 comments:
Post a Comment