Entertainment


NJIA ZA KUJIZUIA KUTOSHIRIKI TENDO LA NDOA KABLA YA NDOA



NJIA ZA KUJIZUIA KUTOKUSHIRIKI MAPENZI /SEX KABLA YA NDOA..! 

Katika Somo lililopita tuliangalia madhara ya kushiriki sex kabla ya ndoa, leo twende tukaangalie jinsi gani mtu anaweza kujizuia kufanya mapenzi kabla ya muda Ulioamriwa..

(1).Kutokuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi mapema.

Ni muhimu kufahamu kila jambo lina wakat wake jambo linaweza likawa jema kabisa lakini kwa kushindwa kuzingatia ni wakat gani unatakiwa ulifanye jambo hilo linaweza likapoteza maana na kuonekana si jema tena.

Ni vizur kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi pale umri na majira yatakaporuhusu, si jambo la busara kwa mwanafunz mfano wa sekondari akawa ana mchumba kwa lengo la kufungua nae ndoa.

Kuna wakat wa kusoma na kuna wakat wa kuanza maandalizi ya ndoa. Labda kama hana malengo ya kuendelea na masomo.

(2).Kutokaa kwenye uchumba kwa muda mrefu.

Uchumba wa muda mrefu ni moja ya kishawishi cha kufanya mapenzi kabla ya muda unaostahiri. Unaweza ukawa na umri sahihi kabisa wa kuoa au kuolewa lakini kama si majira sahihi (bado haujipanga kimaisha) itapelekea muwe na kipindi kirefu cha uchumba ambapo kuzini ni moja ya matokeo yanayoweza kujitokeza.

Ingawa kuna changamoto ya kutaja uchumba unapaswa usizidi muda gani kwa kuwa hakuna muongo rasmi kibiblia ila hekima itabidi itumike kuamua.

Kwa upande wangu napendekeza uchumba usizidi mwaka mmoja (tangu mfahamiane mpaka muingie kwenye ndoa), uchumba wa zaidi ya miaka 2 na kuendelea ni mtego wa kuanguka kwenye dhambi.

(3).Epuka mazingira ya faragha.

Ili kujizuia kutokushiriki kwenye mapenz katika kipindi cha uchumba jitahid kuepuka mazingira ya uficho kama kuwa chumban wawili au kwenda sehemu ya mbali /ugenini mkiwa peke yenu.
Mabint wengi wanajikuta wamezini kwa kudanganywa na vijana wa kiume kuwa waende kuwatembelee chumbani kwa lengo la kuwasalimia au kulala chumba kimoja mfano guest house wakiwa safarin au ugenini kwa kuahidiwa HAWATAFANYA kitu kibaya.

Hivi inawezekana Simba na swala wakakaa chumba kimoja, na swala akawa salama? Sijui labda inawezekana. Ila Usiijaribu sumu kwa Kuilamba.

(4).Epuka kuishi maisha Ya ndoa kabla ya ndoa.

Hapa unakuta binti anaenda kwa kijana wa kiume nyumbani kwake au hostel (kama wapo chuon) kumfulia, kupika, kufanya usafi na Kazi nyingine za ndani. Kama mnaishi maisha haya Jua dhambi ipo Mlangoni Inawasubiri. Watu tuliokoka hatuishi hivyo hayo ni maisha Ya watu wasiookoka.
Kama huyo mwanaume anataka mpaka umfanyie mambo hayo ndio aamini kama unampenda basi akutakii Mema. Ipo siku atasema mlale nae ndio ataamini kweli unampenda au usishangae akakubaka kabisa. KUWA MAKINI.

(5).Uchumba wenu Usiwe wa SIRI.

Haina maana kuwa mara mnapoanza uhusiano muuweke wazi, ila kama kweli mnapendana na mmeamua kuishi maisha ya ushuhuda basi ni vizur ndugu angalau mmoja mwenye hekima ajue.
Hii itawasaidia kuwa na eneo la kukutania pindi mnapotaka kuongea badala ya kujificha vichochoroni na kwenye sehemu za starehe bar, guest house nk.

(6).Kuwa makini na Marafiki ulionao.

Ni hatari kuwa na rafiki ambaye yeye swala la kufanya mapenzi ni jambo la kawaida, hata kama utakuwa na msimamo ushawishi wake unaweza ukakufanya ubadili msimamo wako.

"Chuma hunoa Chuma, Ndivyo mtu Aunoavyo Uso wa Rafiki Yake "

                          MITHALI 27 : 17

Rafiki wa mzinzi ni mzinzi. Rafiki yako alivyo ndivyo ulivyo.

(7).Kuwa Makini na mambo Unayoangalia na Kusikia.

Kama ni mtu wa kupenda kuongelea mambo ya mapenzi mara kwa mara, au ni muangaliaji Mzuri wa Picha za utupu (ponography) basi usishangae kujikuta Ukianguka kwenye uzinzi.

"Jicho lako la kuume likikukosesha, Ling'oe Ulitupe Mbali Nawe, kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala Mwili wako Mzima USITUPWE KATIKA JEHANAMU "

                                    MATHAYO 5 :29

(8).Epuka Kuamshana Hisia za Kimapenzi.

Kwa watu walikuwa kwenye uhusiano ni vigumu kukaa bila kuchezeana /kutomasana Miili. Lakini kama mnataka kuwa na ndoa yenye ushuhuda na Mungu awe katikati yenu INABIDI Mjizuie.
Unaweza ukasema hatutasex ila tunakis, huge basi. Lakini leo huge, kesho kiss, kesho kutwa mkono kwenye paja au kifuani, mtondogoo mtajikuta Mmekula tunda.

MLAMBA ASALI HUCHONGA MZINGA.

(9).Wekeni Msimamo kuwa hamtashiriki Sex kabla ya Ndoa.

Ili kufanikiwa katika hili wote INABIDI Mnie kuwa hamtafanya sex mpaka pale muda ukifika. Kama mwenzako anakushawishi msex kuwa nae makini huyo anaweza akawa ni mjumbe wa shetani kwako na si mume au mke ambaye BWANA amemkusudia.

KAMA HATAKI KUSUBIR BASI MUACHE AENDE, BAKI NA YESU WAKO. 

(10).Jishughulishe na Mambo ya Mungu.

Kujiweka busy na mambo ya Mungu ni moja ya njia ya kujiepusha na mambo Maovu.
Mfalme Daudi alijikuta akizini na mke wa Uria kwa kutokuwa katika vita na badala yake alikuwa tu nyumbani bila ya kuwa na shughuli ya kufanya. 1 SAMWELI SURA YA 11.

"An idle mind is the workshop of the Devil "

*****//**********//****/***/******

UNATAKA KUWA NA UCHUMBA ULIO NA USHUHUDA MZURI NA NDOA YENYE BARAKA ZA MUNGU? FUATA MAMBO HAYA.

KAMA UMESHASEX UKIWA KATIKA UCHUMBA, TUBU DHAMBI HIYO NA TAFUTA MSAADA ZAIDI KWA WATUMISHI WA MUNGU.

NA KAMA BADO UPO SAFI, ENDELEA KUJITUNZA UFIKIE NDOA ILIYO NA BARAKA ZA MUNGU.

MUNGU AKUBARIKI.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.