MAVAZI YAKO YANAKUTAMBULISHAJE.?
MAVAZI YAKO YANAKUTAMBULISHAJE..?
Unapokwenda dukan kufanya shopping ya nguo ni kitu gan unachokiangalia? Unapokwenda kwa fundi kushonesha nguo ni vigezo gani unavyompa? Unataka nguo yako iweje? Kwanin unataka iwe hivyo unavyotaka iwe? Unafahamu hiyo nguo unayotaka kununua ilitengenezwa kwa watu wa aina gani? Na ivaliwe katika mazingira gani..?
Mavazi yana nafsi kubwa sana katika maisha yetu, mavazi yanabeba 'personality' yetu, mavaz yanabeba utambulisho wetu, mavazi yanawapa watu taswira ya tabia zetu na FIKRA zetu zilivyo, watu wanaweza kutufahamu sisi ni watu wa aina gani kupitia tu mavazi yetu. Mavazi ni 'identity' /kitambulisho chetu. Mavazi yako yanakutambulishaje?
Ni jambo la kawaida kwa sasa kumuona mdada amevaa nguo inayoonyesha mapaja yake, matiti yake, kiuno na hata nguo zake za ndani bila kizuizi chochote na yeye akiwa hana habari yupo tu na mambo yake. Huwa nashindwa kuelewa, sijui huwa wanajisikiaje kuvaa hivyo? Hivi wao wanajiona wamevaa suti au? Hivi ni kweli hawaoni shida kuwa hivyo alivyo? Hivi wanafahamu hayo mavazi yanawatambulisha vipi kwa watu?
Naomba niseme hili, mavazi yanabeba utambulisho wa mtu.. Ukiomuona askar akiwa kazini haina haja ya kuuliza kama yeye ni askar au mwalimu? Ukimuona daktar pia utamfahamu kwa koti refu jeupe na kitu kama manati akiwa ameweka shingoni mwake, Ukimuona mchungaji, rubani wa ndege na watu wa kada mbalimbali wakiwa katika maeneo yao ya Kazi ni mavazi yao yanayowatambulisha bila hata wao kujitambulisha. Vipi Ukimuona mdada amevaa sket iliyoacha mapaja yake yote wazi, matiti yapo nje yanachungulia utafikiri embe zinataka kudondoka mtini, nguo yake ya ndani inaonekana michirizi mpaka rangi, anapotembea makalio yanatikisika kama matairi ya gari bovu lililokosa muelekeo, utafikiria ni nani? Utadhani ni askar? Vipi mwalimu? Au daktar?.. Bila shaka huyu atakuwa ni KAHABA (mwanamke anayejiuza).
Naomba niwasaidie dada zangu katika hili, wapo makahaba wa aina mbili, makahaba wanaofanya ukahaba wa kujiuza kingono na wapo makahaba ambao ni makahaba wanaiuza miili yao kwa kutamanisha watu hata kama si kwa ngono. Wote hawa ni makahaba, wametofautiana tu katika sera zao na utendaji wao wa kazi.
"Na tazama, mwanamke akamkuta ana MAVAZI YA KIKAHABA, mwerevu wa moyo " Mithali 7 : 10
MAVAZI YA KIKAHABA NI YAPI?Mavazi yoyote yanaacha maumbile yako ya ndani wazi ni mavaz ya kikahaba. Ukivaa nguo inayoacha maumbile yako nje wewe ni KAHABA hata kama haujiuzi kingono, mavazi yako yanakutambulisha hivyo na ndivyo ulivyo.
Haijalishi kama ni suruali au sketi au nguo ya aina yoyote ile, ili mradi nguo hiyo haisitiri maumbile yako vizuri inavyostahili hiyo ni nguo ya kikahaba. Na kama umevaa mavazi ya kikahaba wewe ni KAHABA sio daktar, polisi au fundi makenika.
Ebu wanawake mfike hatua mjitambue na mjiheshimu angalau kidogo. Kumbuka mavazi unayovaa si kwa ajili yako bali ni kwa ajili ya watu wengine na jamii inayokuzunguka. Unapendeza si kwa ajili yako ila kwa ajil ya wale wanaokuona na nguo nzuri au mbaya si wewe unayeona ila ni watu wanaionaje nguo hiyo.
Kama Unapendeza kwa ajil yako na si wengine, kwanin siku usiamue kuvaa nguo yako nzuri ya gharama unayoipenda na ukashinda ndani siku nzima halafu jion ukaivua? Kwanin ukiwa upo tu ndani huna haja ya kufanya make up ya zaidi ya nusu saa kama siku nyingine unapokuwa na mtoko? Kwanin usitoke tu na kanga yako na zile yeboyebo zako siku ukialikwa kwenye sherehe? Ni kwa sababu mavazi si kwa ajili yako ila kwa niaba ya wengine.
Kama ni hivyo kwanin uvae kaptura ukiwa unatoka? Kwanin uvae night dress wakati wa mchana ukiwa barabarani? Unataka watu wakueleweje? Hivi huo mwili wako ni maonesho? au ni mali ya umma? Mwili wako ni kwa ajil yako na hasa kwa ajili ya mume wako na si wengine. Mtunzie hiyo mali yake, mi sidhan kama atapenda kushare na wengine. Jaribu kumfanya ajisikie fahar kuwa na mwanamke anayejiheshimu na si kahaba.
Kumekuwa na michepuko mingi siku hizi kutokana na kuongezeka kwa wimbi la makahaba wa mavazi. Wanaume wengi wamekuwa waathirika wa kupungukiwa nguvu za kiume kutokana na kuongezeka kwa makahaba wa mavazi, hivi kama mwanaume tangu asubuhi mpaka jion anashinda akiona matiti, viuno, matumbo, mapaja ya wanawake mbalimbali unategemea atakaporudi kwa mke wake atakuwa na hamu naye? Hamu itoke wapi wakati ameshamaliza haja zake katika suruali yake akiwa anawaona makahaba huko nje.! Hana nguvu tena ya kumridhisha mke wake.
Hata wanaume pia nao huvaa mavazi yasiyokuwa na heshima kama kata K na model zinazobana kupita kiasi. Nao pia wanapaswa kujirekebisha, lakini naongelea sana wanawake kwa sababu uvaaji mbovu wa wanaume haupo sana na athari yake haidhuru sana jamii zaidi ya kumshushia yeye mwenyewe Heshima lakini athari ya mavazi mabaya kwa mwanamke huleta MADHARA kwa JAMII nzima.
" Mwanamke ALIYEELIMIKA huielimisha JAMII, Mwanamke ALIYELAANIKA huilaani JAMII "
..........................
Tuache mambo ya kuiga maisha Ya kigeni. Tuache kuwa watumwa wa FIKRA kwa kuiga kila kitu kutoka nchi za magharibi.
Uzuri wako si mpaka utembee nusu uchi. Wewe si kahaba, wewe ni mwanamke wa thamani, mke na mama wa watoto wa baadaye.
KAMA WEWE UNAVAA MAVAZI YA KIKAHABA, WATOTO WAKO WATAVAAJE..?
JIHESHIMU, JITAMBUE, JIPENDE, JIKUBALI JINSI ULIVYO.!
"WEWE NI MTU WA THAMANI
"Kabla hujanunua au kuchagua nguo ya kuvaa, JIULIZE maswal haya :Kwanin niichague hii nguo?Nitaivaa wapi? Na kwanin? Watu watanichukuliaje nitakapoivaa? "
FIKIRI KWA KINA, TENDA KWA BUSARA "
0 comments:
Post a Comment