MAMBO 5 YANAYOIPA THAMANI SADAKA YAKO..!
Utoaji wa sadaka ni utamaduni wetu wa kila siku kama
wakristo , Na ndivyo inavyotupasa kufanya hivyo kama Neno la mungu
linavyoelekeza.
Kuna Baraka katika utoaji wa sadaka , Lakini si kila mtu
anayetoa hubarikiwa.Kuna mambo ya muhimu
5 unayopaswa kufahamu katika utoaji wako wa sadaka.
Mambo hayo ni kama yafuatayo..
1.IMANI
Jambo la kwanza na la msingi katika utoaji wa sadaka ,
litakoipa thamani(Kibali) ni imani. Bila imani haiwezakani sadaka yako ikapata
kibali mbele za Mungu , Kwanini Imani ? Kwa sababu sadaka tunatoa kwa Mungu au
miungu wasioonekane.
Ninaposema tunatoa kwa
MUngu naongelea kwa wale ambao wamemuamini Yesu Kristo kuwa Bwana na
mwokozi wao na ninaposema miungu hapa naongelea kwa wale ambo wapo nje ya Yesu
kristo lakini wana vitu vyao wanavyoviabudu na kuamini kuwa vitawasaidia na
kuwapa majibu yao wanayohitaji mfano, matambiko ya kimila,sadaka zinatolewa kwa
wagamga wa kienyeji nk .
Sasa kutokana na ukweli kwamba sadaka hutolewa kwa Mungu au
miungu isiyoonekana hivyo mtoaji wa sadaka hiyo ni lazima AAMINI kuwa sadaka
yake itapokelewa na huyo Mugu au miungu isiyoonekana, KInyume na hapo sadaka
hiyo haitapata kibali kwa huyo anayetaka kumtolea.
Ikumbukwe kuwa ingawa Mungu haonekani lakini yupo mwakilishi
wake anayepokea sadaka hiyo kwa niaba yake , Ndio hawa wachungaji na watumishi
wa Mungu mbalimbali tulionao duniani.Sadaka hio inapotolewa hupokelewa na
wachungaji na watumishi wengine wa Mungu
na hutumika hapa hapa duniani katika shughuli mbalimbali lakini imani yako
ndiyo itakayopokelewa na kuwekwa kumbukumbu
ya kudumu mbinguni na si Pesa/mali
yako uliyoitoa. Mathyo 6:19-20
Hapa ni pa kuwa makini sana na ndio sehemu inayowakwamisha
wakristo wengi wasione Baraka zao ingawa wanatoa sadaka zao.Kama umetoa sadaka
pasipo kuwa na Imani yaani umetoa kwa mazoea kwa kuwa unatoa kila juma,kama
umetoa kwa shinikizo wasikuone hautoi kanisani au umetoa kwa sabbabu ypyote ile
nje na Imani basi sadaka yako itaishia hapa hapa duniani itatumika na kusaidia
kazi iliyopelekwa kwenda kuifanya lakini mbinguni HAUTAKUWA NA HAZINA YOYOTE.
Kama haujisikii kutoa ni Heri usitoe maana hata ukitoa
hautapata kitu mbele za MUngu ,Utakuwa umepata hasara na si faida.
Mungu hana shida ya pesa/mali yako maana vyote viijazavyo duniani ni
mali yake, Mungu anataka umtolee kwa MOYO WA UPENDO na IMANI.
“kwa IMANI Habili alimtolea Mungu dhabibu (sadaka
) iliyo bora kuliko Kaini , Kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki , Mungu
akazishuhudia sadaka zake na kwa hiyo ijapokuwa amekufa angali Akinena”
Waebrania 11:4
2.UTAKATIFU
Mahusiano yako na Mungu ni muhimu sana ili kuleta
KIbali/Thamani katika sadaka yako.Mungu hana urafiki wa na dhambi na hajawahi
kuwa na hatakuja juwa na ushirika na dhambi.
“Tena pana ulinganifu
gani kati ya Kristo na Beliari(Ufisadi)? Au yeye aaminiye ana
sehemu gani na yeye asiyeamini?” 2
Wakorintho 6: 15
Unapaswa kuwa na mahusiano mazuri na MUngu ili sadaka yako
yako iweze kupata kibali,unatakiwa uwe msafi wa moyo.Ninaposema usafi wa moyo
nazumgumzia vipeg=ngele 2 vya muhimu ..;
I.
Jitenge na dhambi : Hautakiwi kuwa mkristo
mwenye mapando yasiyo ya Mungu ndani mwako,Acha dahmbi ,Jitenge na
dhambi,IKimbie dhambi,Kuwa shirika na dhambi ni kuwa ADUI na Mungu.
“Mtakuwa watakatifu kama MIMI(Mungu ) nilivyo
Mtakatifu” 1 Petro 1 : 16
II.
Ondoa Uchungu Moyoni mwako : Uchungu ulionao
moyoni mwako na roho ya kutokusamehe ni kikwazo cha Mungu kupokea Sadaka yako
na Kizuizi cha Baraka zako kutoka kwa Mungu.
“Bali msipowasamehe watu makosa yao , Wala
baba yenu wa hatawasamehe ninyi makosa yenu.” Mathayo 6 :15
Mungu hapokei mtu mwenye dhambi kwa kuwa yeye si wa
dhambi,Ninaposema hapokei haimaanishi kuwa sadaka yako haitapokolewa kwenye
chombo cha sadaka . La hasha..! Kibinadamu sadaka yako itapokelewa na
inawezakana ukapewa sifa na kuonekana umetoa kuliko wote waliootoa kutokana na
uwezo wako wa kipesa au Heshima yako ,Lakini mbele za Mungu hakuna Thawabu ( Baraka yoyote utakayoipata).
Wapo watu ambao wanadhani kwa kutoa kwao sana wanaweza
kubarikiwa na kupata kibali mbele za Mungu bila kuangalia mahusiano yao na
Mungu , Mungu si mganga wa KIenyeji ,Mungu haongwi wala
kupokea rushwa .Hili ni jambo la msingi sana kufahamu kama
Mkristo,Uhusiano wako na Mungu ni muhimu sana kuliko Sadaka zako unazotoa.
Watumishi wa Mungu pia wanatakiwa kuwa waaminifu kuwaelekeza
wakristo ukweli huu bila kuwaonea Aibu bila kujali vyeo vyao au pesa zao, Ni
jukumu lao kuwaelekeza wakristo waache dhambi na kuwakemea pindi wanapoenda
kinyume na mapenzi ya Mungu.Wasikubali
kununuliwa na watu wenye pesa ambao hawataki kuishi maisha matakatifu kwa
viburi vya pesa zao.
Hata hivyo naomba niweke sawa hapa kitu Fulani , Ni kweli
Mungu hapokei sadaka ya mtu mwenye dhambi lakini hii ni kwa wale ambao
wameookoka lakini bado wanaendelea kuishi maisha ya dhambi huku wakifanya
wokovu kama mwamvuli wao kujifichia Uovo wanaofanya ,Ila kwa mtu ambaye
hajaookoka bado hajampokea Yesu kristo anaweza akatoa sadaka yake na
ikapokolewa kama ameitoa sadaka hiyo kwa Imani .
Katika kitabu cha Matendo ya mitume sura ya 10 inaelezea
habari ya mtu mmoja aliyeitwa Kornelio ambaye Mungu alipokea Sadaka zake na
kujibu maombi yake ingawa hakuwa ameokoka , Na kwa sababu ya utoaji wake Mungu
alimpa Neema ya kupokea Wokovu.
Kwa wewe ambaye umeokoka hauwezi kutumia mfano huu wa
Kornelio badala yake unatakiwa kuishi maisha matakatifu ili Mungu akubariki
katika maisha yako .
3.KIWANGO UNACHOTOA.
Kiwango chako unachotoa ni moja ya vitu vinavyoipa thamani
sadaka yako.Ili uweze kunielewa hapa ni vizuri kukumbuka kuwa Mungu hana shida
ya pesa au mali yako , Lakini pamoja na ukweli huu bado anahitaji tutoe sadaka
,Ni kwanini Mungu anahitaji tumtolee sadaka wakati yeye hana shida za Pesa au
Mali zetu.?
Mungu anataka tutoe sadaka ili aweze kupata MIOYO
yetu,Anahitaji tuwe karibu na yeye njia
pekee kubwa ya kupata mioyoyetu ni kupitia kwenye Mali au pesa zetu.Kuna
uhusiano mkubwa sana kati ya mtu na mali yake ,Nguvu hii kubwa ya kimahusiano
kati ya mtu na mali/pesa yake ndio huifanya akati mwingine kuitwa mungu wa
pili.
Hivyo Mungu anatutaka tumtolee sadaka ili tujifunze
kudhibiti mafanikio yetu ,kutufundisha Unyenyekevu na kumtegemea yeye.
“Kwa hazina yako ilipo ndipo moyo wako utakapokuwepo “ Mathayo
6 :21
Hivyo tunapomtolea Mungu hazina (sadaka) zetu tunatoa sehemu
ya mioyo yetu, Na hili ndio lengo la kubwa la Mungu na wala si vile tunavyotoa.
Sasa unapotoa sadaka ni lazima uhakikishe kiasi unachotoa
kinaugusa moyo wa Mungu na si kutoa ili mradi umetoa.Unaweza ukauliza
ninawezaje kufahamu kiwango ambacho kinaugusa moyo wa Mungu kitakachoifanya
sadaka yangu iwe ya Thamani ?
Kujua kiwango ambacho
kitaipa kibali sadaka yako ni kwa kutoa kiasi ambacho moyo wako utajisikia
kuumia ndani yako,Hicho ndio kiwango ambacho unatakiwa kutoa .Ok,labda bado
haujanielewa , Niseme ka lugha nyingine
,Thamani ya sadaka yako haipimwi na kiasi ulichotoa kwenye chombo cha
sadaka bali inapimwa na iwango ambacho
kimebaki mfukoni mwako.
Nitoe mfano wa watu wawili , Mmoja alikuwa ana sh 500 akatoa
sadaka sh 400 na akabaki na sh 100 mfukoni mwake , Na wa pili alikuwa ana sh
10,000 akatoa sh 1000 sadaka na akabaki na sh 9,000 mfukoni mwake ni nani
aliyetoa zaidi ?
Ukiangalia viwango walivyotoa kwenye chombo cha matoleo Yule
wa pili ataonekana ametoa zaidi kwa kuwa ni wazi 1000/= ni kubwa kuliko 400/= ,Lakini mbele za Mungu
Yule wa kwanza ndio aliyetoa zaidi kuliko wa pili , kwanini ? Kwa sababu wa
kwanza baada ya kutoa 400/= alibaki na 100/= hii ina maanisha alitoa pesa yake
karibu yote (80%) wakti Yule wa pili alikuwa na sh 10,000 akatoa sh 1,000 na
kubaki na sh 9,000 ,hii ina maana alitoa sehemu ndogo sana (10%) na kiasi kikubwa alibaki nacho mwenyewe.
Hivyo wa tahamani ya sadaka ya Yule wa kwanza ni kubwa
kuliko Yule wa pili,kwa kuwa ametoa sehemu kubwa ya moyo wake (hadhina) wakati
Yule wa pili alitoa kiasi kidogo tu na sehemu kubwa ya hadhina yake alibaki
nayo mfukoni mwako.
Kupenda ni kutoa kama hautoi haujapenda .Mpe Mungu vile vilivyo
bora akufanye uwe Bora ,ukimtolea mapooza(vitu visivyofaa) na yeye atakufanya
kuwa Pooza (mtu usiyefaa).
Mungu asema hivi;
“Kwa maana wale wanaoniheshimu nitawaheshimu , Na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu “ 1 Samweli 2 : 30
4. MUDA UNAOTOA SADAKA YAKO.
Kuna sadaka zingine zinatakiwa kutolewa kwa kipindi maalumu
ambacho Mungu ameagiza itolewe, Mtoaji anapaswa kuzingatia muda huo na kama
muda huo ukipita basi sadaka hiyo inakuwa haina maana tena .
Sio sadaka zote zimefingiwa na muda Fulani wa kutoa na si
sadaka zote unatoa muda wowote unaojisikia.Na ndio maana ni vizuri kumsikiliza
Roho Mtakatifu ili akupe maelekezo ya ni ni unatakiwa kufanya kutokana na
sadaka yako .
Kuna wakati Mungu anaweza kukupa msukumo wa kutoa sadaka
sehemu Fulani au kwa mtu Fulani ndani ya kipindi Fulani ,Sasa ama kwa kutokujua
nini unaambiwa ufanye au kutokana na ugumu tu wa moyo kuona ukitoa pesa hiyo
unapoteza pesa yako na labda tayari kuna matumizi ambayo tayari umeshaipangia
unaweza usiipeleke sadaka hiyo kwa wakati , Na unakuja kupata wazo la kukubali
kuipeleka sadaka hiyo ukiwa tayari umeshatoka Nje ya muda ulioamriwa, N a hata
ukitoa haitakuwa na Thamani tena, Inaweza ikapokelewa kama pesa na si sadaka.
Sadaka hizi hutokea pale kuna mtu Fulani ana shida ya pesa au
kitu fulani na hana njia ya nyingine ya kuitatua shida hiyo na anaamua kumuomba
Mungu amvushe katika kipindi hicho ,hivyo MUngu anaweza kuleta msukumo ndani
yako wa kwenda kumpatia mtu huyo pesa hiyo ili iweze kumsaidia katika kipindi
hicho anachopitia . Sasa kama ukiwa na moyo mgumu na kugoma kupeleka pesa hiyo
Mungu atamtumia mtu mwingine na wewe baada ya muda utajikuta ule msukumo ndani
yako umepoa kabisa,hali hii inamaanisha muda wa sadaka hiyo umesha EXPIRE.
Sadaka ya namna hii tunaona kipidai ambapo mtumishi wa Mungu
Eliya Mtishbi alipoambiwa aende kwa mjane wa Sarepta ili aweze kupata chakula,
Yule mjane alikuwa na chakula kidogo sana ambacho kilitosha mlo mmoja tu baada
ya hapo alikuwa hana matuamini mengine ya kupata chakula. Eliya alipoenda kwa kwa
Yule mjane alimuambia amuandalie chakula ampe ale ,ingawa Yule mjane hakuwa na
chakula isipokuwa hicho alitii sauti ya Eliya na kufanya kama alivyo muelekeza,
Na baada ya hapo tunaona Mungu alifanya muujiza wa chakula kwenye ile nyu,nay a
Yule mjane na walikula chakula mpaka kipoindi cha ukame kilipofika mwisho.Soma
1 Wafalme 17 : 10-16
Nini tunaona katika habari hii, Hapa tuanona Yule mjane
alitii sauti ya Mungu ndani mwake ya kumpatia Eliya chakula kama
alivyoagizwa.Kama angegoma kufanya hivyo basi Mungu angetengeneza njia nyingine
ya Mtumishi kupata chakula ,Na baadaye Yule mjane angeamua kumtafuta Eliya
asingejua ameelekea wapi, Hivyo thamani ya msaada (Sadaka yake iliuwa muda ule
ule ambao Eliya alimuambia ampatie chakula).
Kitu kingine tunachokiona kwenye habari hii ni kwamba Mungu
anapokuambia umpatie mtu Fulani kitu au pesa basi uje ameandaa kitu kikubwa
zidi kwa ajili yako , ukikubali kutoa utapokea Baraka hiyo ila ukipinga
hautaipata Baraka hiyo na wakati mwingine hata kile ambacho ulijaribu kuzuia
usitoe utakipoteza.
Tii sauti ya Mungu, usikubali upitwe na Baraka yako .
5.MAHALI UNAPOTAKIWA KUTOA SADAKA YAKO.
Jambo la mwisho linaloipa sadaka yako Kibali / Thamani ni sehemu
unayotakiwa kuitoa hiyo sadaka , SI kila sehemu ni sehemu sahihi ya wewe kuto
sadaka yako. ZipoSadaka ambazo zinatakiwa
kutolewa kwa maelekezo maalumu kufuatana na vile Mungu anasema ndani yako na
kama uakatoa sehemu nyingine basi sadaka hiyo haitakuwa na Thamani mbele za Mungu.
Hapa sizungumzii sadaka za kila juma ambazo tunatoa
tunapokutana kwenye ibada , Ninazungumzia sadaka kama Fungu la kumi ,ambayo
unatakiwa kutoa kwa kuhani wako (Mtumishi wa MUngu anayekulisha na kukulea
kiroho) na sadaka zingine pia ambazo Mungu anaweza kukupa maelekezo ni wapi ukaitoe sadaka hiyo , Kwa mfano .Hauwezi kutoa fungu la kumi sehemu yoyote tu unayojisikia wewe ,
Hauwezi kutoa fungu la kumi mahali ambapo haubudu , Hauwezi kutoa fungu la kumi
kwa wajane ,Yatima na watu wenye shida mbalimbali ,huu si utaratibu na ukifanya
hivyo utakuwa umetoa mchango tu kwa hao watu nab ado utabakia na deni la kutoa
fungu la kumi.
Unaweza ukauliza ni kwanini? Sikia ingawa sadaka yako
umeipeleka kwenye ufalme wa Mbinguni lakini umeweka kwenye Akaunti tofauti na
ile uliyotakiwa kuweka. Nitoe mfano mmoja rahisi , Benki inaweza kuwa ni moja
mfano CRDB lakini ikawa na akaunti tofauti za moja , Sasa kama unaenda kuweka
pesa kwa ajili ya malipo ya ada basi weka pesa hiyo katika akaunti husika ukeweka kwenye akaunti yako ya akiba
usitegemee kuwa kupata Risiti /Muamala unaoonesha malipo ya ada na badala yake
utapata risiti inayoonesha umeweka pesa yako kwenye akaunti ya akiba.
Hivyo hata katika utoaji wa sadaka kwa Mungu unapotoa sadaka
kwa ajili ya wajane . Yatima na makundi ya watu tegemezi sadaka yako itasoma
kwenye akaunti tofauti na ukitoa sadaka yako kama fungu la kumi, Ingawa akaunti
zote zipo katika ufalme wa Mungu.
“Usiache kutoa Zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya
mbegu zako,yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka . Naweutakula mbele za BWANA
,Mungu wako MAHALI ATAKAPOCHAGUA apakalishe jina lake………” Kumbukumbu 14
:22-23
Katika mstari huo juu kuna eneo hapo linasema mahali
atakapopachagua , Hivyo kuna baaadhi ya sadaka inabidi zitolewe sehemu maalumu
ambayo Mungu mwenyewe atakapopachagua ,K ama ukitoa bila utaratibu hautaona Baraka
ile ambayo Mungu aliikusudia kwako.
MUNGU AKUBARIKI
MWL JOHN C. NTOGWISANGU
Contacts: Phone -0712463344/0765166702, Email -jcntogwisangu@gmail.com, Watsap 0712463344
Amina nimeokoka
ReplyDelete