Entertainment


THAMANI YA MWANAMKE IPO WAPI?



THAMANI YA MWANAMKE IPO WAPI..?

Hapo mwanzo, mwanamke alikuwa anaheshimika kwa kujitunza mwili wake, ilikuwa ni jambo la ajabu na aibu kwa familia kama binti ataolewa akiwa hana BIKRA. Lakini sasa bikra ni kitu adimu kisichowezekana.

Thamani ya mwanamke kwa sasa imeshuka sana, mwanamke kuvua nguo kwa mwanamke ni jambo la kawaida, kuvua nguo kwa sababu ya pesa, kwa sababu ya kupata Kazi, kwa sababu ya kufaulu mtihani, kupata cheo au nafas ya juu kazin ni hali ya kawaida. Hakuna hofu, hakuna thaman tena ya mwanamke.

Mwanamke amekuwa kama chombo cha starehe, kama kitu Cha kutumiwa na kutupwa.
Hapo mwanzo, ilikuwa ni nadra kuona maumbile ya mwanamke kirahis, wanawake walikuwa wakiitunza miili yao kuliko chochote kile wawezacho kukitunza. Mwili wa mwanamke ulikuwa unafunikwa na mavazi ya heshima kuanzia kichwani mpaka miguuni, si kwamba walikuwa hawajui kuvaa, si kwamba walikuwa hawapendezi.. La hasha! Walikuwa wanapendeza na kulikuwa na mitindo mbalimbali ya mavazi lakin ilikuwa ya heshima. Walifahamu thamani ya miili yao, walijiheshimu na walijitunza.

 Lakini sasa kuona mapaja, matiti, kiuno na sehemu nyingine za mwanamke ni kama vile kuangalia maonesho ya sabasaba kila kitu kipo wazi, ushindwe wewe tu macho yako. Ukitaka weupe, maji ya kunde, weusi, wale wembamba, wanene yaan type zote.. Kila kitu ni laivuu bila chenga. Its free a half ponography.

 Kuvaa nusu uchi ndio fasheni, tena wanawake wanashindana huyu akiacha titi wazi, mwingine anaachia paja yaan ni kama ligi ya vodacom simba na yanga. Hakuna maadili, watu wanaenda na wakati. Labda niwasaidie dada zangu, kusudi la kwanza la mavaz ni KUSITIRI mwili kupendeza ni jambo linafuata. Lakini sasa kupendeza na kutaka kuonesha maumbile ya ndani ndio jambo la kwanza habar ya kusitir mwili waachie wazee.

Heshima, unyenyekevu na utii ndio lilikuwa pambo kubwa kwa mwanamke na ndio vitu vilivyoangaliwa kama mojawapo ya vigezo vya msingi ili binti aweze kuonekana anastahili kuolewa. Lakini sasa kupata sifa hizo ni kama mchezo wa ku Bet, ni bahat nasibu.

Niliwah kusema wanawake wengi wa sasa vazi la suruali wanalipenda si kama fasheni tu bali hata AKILI zao pia zimevaa suruali. Wana mawazo ya kutaka kushindana na wanaume, hawataki kujishusha, hawataki KUONGOZWA ni wanawake-wanaume (double sex). Tena kwa bahat mbaya awe amesoma au ana pesa kumzidi mwanaume hapo Kazi ipo. NI SHIDA.

Asili ya mwanamke ni Upendo na ukarimu kwa mume wake watoto na ndugu kwa ujumla. Lakini sasa upendo wa mwanamke upo palipo na pesa, kama hamna pesa hamna upendo. Pesa imekuwa ni kila kitu kwa wanawake wa sasa, mwanaume asiyekuwa na pesa, asiyekuwa na gar au Kazi nzuri hana soko kwa wanawake. Pesa inaongoza na kutawala moyo wa mwanamke .

 Mwanamke ndiye kiunganishi kati ya ndugu wa pande zote mbili (upande wa mwanamke na mwanaume), lakini wanawake wengi wa sasa wapo kimaslahi wanajali upande wa kwao na kusahau upande wa mwanaume.

Kutoa mimba kwa sasa ni kitu rahisi kama kwenda kuoga bafuni na kurudi. Binti wa miaka 16 unakuta ametoa mimba zaidi ya moja, akifika miaka 28-30 atakuwa ametoa ngapi? Ndio hawa wanakuja kusumbua kwenye ndoa kwa kushindwa kuzaa. Kama umeshatoa mimba 4 au 5 unataka uzae ili iweje? Haujui hizo mimba ulizotoa ni watoto hao? Mi sioni umuhimu wa kuzaa tena, watoto wako ndio hao uliowaua mwenyewe, subiria ukifa utawakuata huko wakikulia kwanin ulikatisha maisha yao? Kwanin hukuwapa haki ya kuiona dunia? Kwanin hukuwa tayar kuwalea. Kile unachopanda ndio unachovuna. KAA BILA MTOTO. USISUMBUE WATU.

Kujitongozesha kwa wanawake wa kizaz hiki ndio staili, mwanamke utakuta anajipitisha pitisha mbele za wanaume mpaka apigiwe "pssssss, sister mambo? Umependeza.! " ndio ajisikie raha. Mi naona ni kukosa KUJITAMBUA, kwani uzur wako mpaka upigiwe miluzi kama mbwa? ACHA KUJIRAHISISHA. JIHESHIMU. Kumbuka "kizuri chajiuza, kibaya........?"

***************
Nina mengi ya kuongea lakini naomba niishie hapa kwa leo. Kama ni mtu wa kuelewa naamini utakuwa umeelewa. Sikulazimishi kukubaliana na mimi ila naamin ujumbe umefika. KAZI KWAKO.

MWANAMKE NI MTU WA THAMANI SANA.

JITAMBUE, JIHESHIMU, JIKUBALI, JIAMINI, JITUNZE KWA AJIL YAKO, MUME WAKO NA WATOTO WAKO.

ACHA MAMBO YA KUIGA, ACHA MAMBO YA KWENDA NA WAKATI.. ACHA WAKATI UENDE.. WEWE BAKI NA HESHIMA YAKO.

# WANAWAKE MNAWEZA MKIJITAMBUA #
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.