NI WAPI NITAMPATA MKE AU MUME
MWEMA..!
Wapi ninaweza kumpata mke au mume
mwema? Hili ni swali ambalo kama kijana nadhan ulishawahi kujiuliza au
ulishawahi kuulizwa na mtu wako wa karibu.
Kabla hatujaenda kuangalia ni wapi
unaweza kumpata mke /mume mwema, ebu tuangalie mke /mume mwema ana sifa gani?
Au unawezaje kumtambua mke /mume mwema? Vigezo vya kuchagua mke au mume
vinatofautiana kwa mtu na mtu lakini mke au mume mwema huwa wanasifa kuu mbili
(2) :
(1). UPENDO , mtu anayestahili kuwa
mwenzi wako wa maisha anapaswa kuwa na upendo wa dhati kwako, kama huuamini
upendo wake au huna uhakika kama ana upendo wa kweli au la, huyo hakufai
usipoteze muda wako kwake. Unaweza ukajiuliza nitajuaje kama ana upendo wa
kweli? Jibu la swali hili ni rahisi sana, mtu anayekupenda atatoa muda wake
kwako kwa kuwa nae karibu kwa kukutoka wote, kukupigia simu, kujibu text zako
kwa wakati, kujitoa kwako pale unapokuwa na shida, kukuheshimu, kukusikiliza,
kukutii na mambo mengi kama hayo ili mradi akuone upo na furaha.
Watu wametofautiana viwango vya
kujitoa hivyo usimfananishe mwenzi wako uliye nae sasa na yule aliyepita au
kumlinganisha na mpenzi wa mtu mwingine. Jambo la kuzingatia hapa ni hili
"UPENDO NI KUJITOA", Hivyo mtu anayestahili kuwa mwenzi wako wa
maisha anapaswa kujitoa kwako na wewe mwenyewe ndio utakuwa shahidi juu ya
kujitoa kwake kwako (haina haja ya kumuuliza mtu mwingine).
(2).KUENDANA NA MALENGO YAKO NA AINA
YAKO YA MAISHA ..!
Hili pia ni jambo la msingi sana kuzingatia, mume au mke
unayepanga uwe nae ni LAZIMA awe anakufahamu na unamfahamu vizuri hasa kwenye
mambo anayopendelea kuyafanya na aina yake ya maisha kama yanaendana na maisha
yako.
Mahusiano mengi ya vijana ya sasa
hayadumu kutokana na wapenzi kukosa muda wa kuchunguzana kwa UNDANI kabla ya
kuanzisha mahusiano, wengi wamekuwa na maamuzi ya haraka yanayoongozwa na hisia
na tamaa ya macho. Mke au mume anapaswa kuwa ni mtu anayekufahamu na
unayemfahamu vizuri kwa kuwa pindi mnapoanza kuishi pamoja ni TABIA zenu
zitakazo wafanya mfurahie maisha yenu au kuona maisha yenu ni mzigo hata
kufikia KUACHANA.
Mke au mume mwema ni RAFIKI MWEMA,
Najua hauwezi kuwa na rafiki wa karibu ambaye hamfanani mambo mnayopendelea
katika maisha (Hobbies and interests) kadhalika huwezi kuwa na mke au mume
mwema ambaye mmetofautiana vipaumbele vya maisha. Ukisema unampenda tu hata
kama mmetofautiana katika vipaumbele na mtindo wa maisha fahamu kuwa mahusiano
hayo hayatadumu na yatapotea hewani kama upepo.
Uchumba mzuri ni vizuri ukaanzia
kwenye urafiki, na uchumba wenye ushuhuda mzuri na uliokubalika na wazazi wa
pande mbili na Mungu pia akiwa katikati huleta NDOA NJEMA.
Ni vizur kupitia hatua hizi urafiki,
uchumba na hatimaye ndoa ili mpate muda mwingi wa kuelewana kwa undani kabla ya
kufikia UAMUZI wa KUFUNGA PINGU ZA MAISHA, ukikosea kwenye ndoa umekosea maisha
yako yote na si rahis kutoka (kama ni mkristo uliyeokoka) na ndio maana ikaitwa
pingu za maisha au kifungo cha maisha.
Upendo na kuendana aina na
vipaumbele vya maisha ni nguzo kuu za kujenga NDOA IMARA bila kusahau Mungu
kama ni muanzilishi wa safari hiyo. Sifa zingine kama elimu, kabila, urefu,
ufupi, unene, rangi ya mtu ni sifa za ziada, Hivyo kuwa makini usije ukafanya
sifa za ziada kuwa ni VIGEZO VYA MSINGI NA VIGEZO VYA MSINGI KUWA SIFA ZA
ZIADA.
Tukirudi kwenye swali letu la msingi
kuwa ni wapi unaweza ukampata mke au mume mwema? Jibu la swali hili anafahamu
Mungu pekee, kuoa au kuolewa kunapangwa na Mungu na hata eneo na wakati wa
kukutana na mwenzi wako upo chini ya Mungu.
Unachotakiwa kufanya ni kujiandaa na
kuendelea kuomba, kumbuka kuepuka maamuzi ya kukurupuka na kusema Mungu
amekuonesha wakati ni TAMAA zako ndizo zilizokuonesha.
MUNGU HADHIHAKIWI.! MATOKEO YA
MAISHA YAKO YATATEGEMEA NA MKE AU MUME UTAKAYE MUOA AU KUOLEWA NAYE.
NAKUTAKIA MAANDALIZI MEMA YA NDOA
YAKO.!
0 comments:
Post a Comment