NINAWEZA KUOA AU KUOLEWA NA MTU ASIYEAMINI (ASIYEOKOKA)..?
Leo ningependa kungalia upande wa kuoa /kuolewa na mtu asiyeamini, kama
kijana unaweza ukawa umekutana na swali hili ambalo tutaenda kuliangalia kwa
upana wake na kama si wewe basi hata ndugu au rafik yako wa karibu anaweza
akawa yupo kwenye kipindi cha kujiuliza swali hili.
Katika mazingira au jamii yetu tunakutana na watu wa aina mbalimbali kipindi
tukiwa mashuleni, vyuoni, kazin au sehemu nyingine katika jamii, na katika
mazingira hayo tunaweza tukajikuta tukiwa tumependa watu ambao si wa imani
yetu, si watu waliokoka. Je tunafanyaje? Na tukiangalia tunapendana sana na
hakuna shida yoyote kati yetu isipokuwa utofaut wa imani zetu tulizonazo.
Biblia inasemaje kuhusu hili?
Naomba nianze kwa kunukuu andiko hili 2 WAKORINTHO 6:14 - 18,tutaangalia
mstar 14 & 15,
"Msifungiwe NIRA pamoja na wasioamini kwa jinsi isivyo sawasawa kwa
maana pana urafik gani kati ya HAKI na UASI? ,
'Tena pana shirika gani kati ya NURU na GIZA? Tena pana ulinganifu gani kati
ya KRISTO na BELIARI (ufisadi)?
' AU YEYE AAMINIYE ANA SEHEMU GANI PAMOJA NA YEYE ASIYEAMINI? "
Maandiko hayo yanazungumzia habar ya mtu aliyeokoka kuoa au kuolewa na mtu
asiyeokoka, Neno NIRA limetumika kuelezea muunganiko wa mwanamke na mwanaume wa
ndoa.
Nira ni kitu ambacho kilitumika kuwaunganisha wanyama (hasa ng'ombe) kwa
kuwafunga kitu hicho shingoni ili waweze kwenda kwa pamoja bila kuachana, mara
nying hutumika katika kilimo ili kuwafanya wafanye Kazi hiyo pamoja, hata kama
mmoja akichoka basi Nira hiyo itamfanya aendelee na Kazi kwa kulazimishwa na
mwingine, Hivyo Nira unaweza pia ukaiita ni KIFUNGO kwa kuwa kinamkosesha uhuru
wa mmoja kati ya wanyama hao kufanya maamuz yake binafsi.
Kupitia Nira wanyama wawili wanakuwa si wawili tena bali ni mwili mmoja.
Ukiangalia kwa ukaribu Nira inavyotumika ni sawa na neno NDOA tunavyolitumia
pindi watu wanapounganishwa madhabahuni.
Baada ya ndoa watu wawili wanakuwa si wawili tena bali ni mwili mmoja, baada
ya ndoa mmoja hata kama akitokea amechoka kuendelea na ndoa hiyo si rahisi
kutoka kwa sababu ndoa imewaunganisha na hairuhusu kuachana, Hivyo hapa pia
NDOA unaweza ukaiita KIFUNGO kama tulivyoona NIRA ilivyotumika, na ndio maana
ndoa huitwa kwa jina lingine PINGU ZA MAISHA.
Kutokaa na andiko tulilolisoma hapo juu ni wazi kabisa hatutakiwi kufanga
ndoa au kufungiwa Nira na mtu ASIYEAMINI /ASIYEOKOKA. Najua unaweza ukawa upo
kwenye uhusiano na mtu ambaye HAJAOKOKA na unampenda sana hivyo kwa kusema hivi
ninaweza nikawa nakuumiza sana moyo wako na kukukatisha tamaa, lakini sina
jinsi kama huu ni UKWELI sina budi kuuleza kama ulivyo bila kificho ili
nikusaidie usimkosee Mungu, na kwa kufanya hivyo nitakuwa nimekusaidia pia
Mungu atanibariki kwa kuiokoa Nafsi yako iliyo ya THAMANI SANA mbele zake.
Tangu katika agano la kale Mungu akiwakataza watu wake wasioe au kuolewa na
watu wa jamii nyingine nje ya Israel, kama ilivyo sasa tusivyotakiwa kufanya
hivyo
.
Hata Ibrahimu alipotaka kumtafutia mke mwanae Isaka alimuagiza mtumishi wake
kwa kumuapiza kuwa asiende kumchukulia mke katika jamii ya watu ambao si wa
nyumban kwake,
MWANZO 24 :1-4
"Basi Ibrahimu alikuwa mzee mwenye miaka mingi na BWANA alikuwa
amembariki Ibrahimu katika vitu vyote. Ibrahimu akamwambia mtumishi wake mzee
wa nyumba yake aliyetawala vitu vyake vyote,
'TAFADHALI UUTIE MKONO WAKO CHINI YA PAJA LANGU NAMI NITAKUAPISHA KWA BWANA,
MUNGU WA MBINGU NA MUNGU WA NCHI KWAMBA HUTAMTWALIA MWANANGU MKE KATIKA BINTI
ZA WAKAANANI AMBAO NAKAA KATI YAO,
'BALI ENENDA HATA NCHI YANGU NA KWA JAMAA ZANGU UKAMTWALIE MWANANGU ISAKA
MKE "
(ni vizur ukisoma sura yote......)
Hivyo swala la kuoa /kuolewa nje ya watu wa jamii yetu (waliokoka) ni
KINYUME cha Neno na mapenzi ya Mungu. Unaweza ukawa ulishasikia hili, lakini
labda unajiuliza ni kwanin Mungu akataze? Shida ipo wapi? Naomba nikaelezee
sababu kama 4 hivi :
(1). KUZAA MATUNDA.
Mungu alipotuchagua, alkusudia tumzalie matunda katika wokovu wetu na hii
ndio sababu ya sisi kuwepo duniani.
YOHANA 15 :16,
"SI ninyi mlionichagua mimi bali ni mimi niliowachagua ninyi nami
nikawaweka mwende MKAZAE MATUNDA na matunda yenu yapate kukaa ili kwamba lolote
mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni. "
Pia ukisoma katika MWANZO 1 :28, alipomuumba Adam na Hawa aliwaambia ZAENI
mkaongezeke, hapa alikuwa hamaanishi tu kuzaa watoto na kuongezeka kwa idadi ya
kawaida bali alikuwa anamaanisha KUZAA NA KUONGOZEKA KIROHO.
Mungu anapokupa mke au mume haangalii tu mwende mkazae watoto wa kimwili
bali pia huangalia KUSUDI lake alikoweka ndani yenu la kitumishi, Hivyo
huangalia matunda yenu mtakayozaa kiroho pindi mkiwa pamoja.
Si kila mtu anaweza akakusaidia kutimiza kusudi la Mungu ndani yako, Hivyo
unabidi utulie ili akupe mtu sahihi. Hata kama ameokoka si sababu ya yeye
kukufanya umtumikie Mungu kama yeye alivyopanga.
Sasa kwa mtu asiyeokoka ni WAZI kabisa hawezi kukusaidia katika hili.
(2).MWILI WAKO NI HEKALU LA MUNGU
.
Miili tuliyonayo ni hekalu la Mungu kwa kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yetu
hivyo hatuwez tukaangunisha miili yetu ambayo ni hekalu la Mungu na miili ya
watu wasiokoka ambayo ni hekalu la miungu mingine. Kufanya hivyo ni dhambi na
chukizo mbele za Mungu.
Kumbuka hekalu ni sehemu /nyumba ya ibada hivyo huwezi ukamchanganya Mungu
na miungu mingine katika ibada ya pamoja, ni lazima mmoja kati yao aondoke.
Usisahau pia watu wakiwa kwenye ndoa wanakuwa mwili mmoja yaani unachanganya
mwili wako ambao ni Mtakatifu na mwili wa mtu mwingine asiyeokoka ambao
usiomtakatifu.
Soma 1 WAKORINTHO 6 :19
(3).NDOA INA NGUVU YA KUGEUZA MOYO WAKO.
Kama ukioa au kuolewa na mtu ASIYEAMINI kuna uwezekano mkubwa wa wewe
kushindwa kumwabudu Mungu na kuacha WOKOVU.
Mfalme Sulemani alipoanza kumtumikia Mungu alikuwa na juhudi na moyo wa
kumpenda sana Mungu lakini alipokuja kuoa wanawake wageni (wasiookoka) aliacha
kumtumikia Mungu wa kweli na akatumikia miungu migeni ya wake zake.
Soma 1 WAFALME 11 :1-3.
(4).NDOA INA NGUVU YA KUKUFANYA UENDE MBINGUNI AU JEHANAMU.
Ndoa si kitu Cha kuchezea, si kitu Cha majaribio, ndoa itakufanya uende
mbinguni au ukose kumuona Mungu. Hivyo usijaribu KURAHISISHA UAMUZI wako wa
nani wa kuingia nae kwenye ndoa.
FIKIRI KWA MAKINI, AMUA KWA BUSARA.
*********//*********, ***//, ********
Kama upo kwenye ndoa ukiwa bado wote hamjaokoka lakini baadae ukawa umeokoka
maandiko yanasema usimuache mwenzako hata kama yeye hajaokoka kama yupo tayar
kuendelea kuwa na wewe. 1 WAKORINTHO 7 :12-16.
Na kama ulifanya kosa la kuoa /kuolewa na mtu asiyeokoka ukiwa wewe upo
kwenye wokovu, INABIDI utubu dhambi hiyo kisha utafute msaada zaidi kwa
watumishi wa Mungu.
Na kwa wale ambao wameokoka ila wana wachumba ambao hawajaokoka, si mimi
bali Mungu anawaambia MSIFANYE KOSA /DHAMBI YA MAKUSUDI YA KUOA AU KUOLEWA NA
MTU ASIYEAMINI
EZRA SURA YA 10 (soma hapa)
Ni kweli unampenda sana na yamkini mmetoka nae mbali lakini kumbuka upendo
wako kwa Mungu UNAPASWA kuzid upendo wako wa kibanadamu na Yesu umetoka nae
mbali kuliko huyo mpenzi wako.
Amekuahidi atabadilisha dini? Ndugu wokovu si DINI ila ni KUCHAGULIWA, ni
UTAKATIFU KATIKA KRISTO YESU.
SHINDA MOYO WAKO, FANYA UAMUZI SAHIHI.
SIKU ZOTE MOYO NI MDANGANYIFU...!
USIUCHEZEE WOKOVU WAKO.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment