Entertainment


MISINGI 10 YA NDOA ISIYO SALAMA



MISINGI 10 YA NDOA ISIYO SALAMA..!

Usioe /kuolewa kwa sababu... :

(1).Umri unaenda. 

Ni heri uchelewe kufika, kuliko kuwahi kujuta.

(2).Ya mimba. 

Mimba si kiashiria cha upendo. Mimba inaingia siku moja lakini ndoa ni ya maisha.

(3).Muonekano.

Uzuri ni wa muda tena hufifia, tabia hudumu daima.

"uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti ".

(4).Msukumo wa wazazi. 

Ndoa ni yako na si ya wazazi, machungu au furaha ya ndoa hiyo ni wewe utakaye yaona. Wao walipanga yao ni zamu yako kupanga ya kwako.

(5).Kumuonea mtu Huruma.

Kutokumpenda mtu sio dhambi na hakuna adhabu juu yako kwa kushindwa kumpenda. Usijilazimishe tafuta mtu ambaye ni chaguo lako.

(6).Tamaa ya pesa na matarajio ya maisha mazuri.
 
Pesa na maisha hutafutwa, ila upendo ni asili (natural). Upendo haununuliwi, haupimwi kwa pesa. Kumbuka, wewe sio bidhaa bali ni mtu wa THAMANI, usijirahisishe.

(7).Kutaka kupata mtoto. 

Ndoa si mtoto, watoto ni matokeo ya ndoa. Unaweza ukapata mtoto ukakosa ndoa na unaweza ukapata ndoa na ukakosa mtoto. Subir, acha haraka.

(8). Kuoa /kuolewa na mke au mume wa mtu. 

Mapenzi hayachanganywi. Mapenz hawa'shei', mapenz hawaazimani, mapenz sio nguo. Acha kujiingiza kwenye mtego wa kujitakia mwenyewe. Subir, upate wa kwako. Kuwa mpole.

(9).kuoa /kuolewa ili umuumize Ex - wako.

Ndoa si mashindano. Furaha au machungu ya ndoa yako utayabeba wewe na si Ex wako. Waza kwa Busara.

(10).Kuoa /kuolewa na mtu asiye muaminifu. 

Usijipe moyo, kama ameshindwa kuwa mwaminifu sasa atakuwa mwaminifu baada ya ndoa? Usidanganyike.. Nyota njema huonekana asubuhi.!

MWISHO : IPO MISINGI MINGI YA NDOA ISIYO SALAMA. HAPA TUMEANGALIA MICHACHE TU.
 
JAMBO LA KUZINGATIA NI HILI, NDOA SI MAJARIBIO, NDOA SI KITEGAUCHUMI, NDOA SI TAMASHA LA MAONESHO WATU WAKUSIFIE.. NDOA NI MAISHA YAKO NA HATIMA YAKO..! 

***You can choose an angel and live in PARADISE or You can choose a Devil and live in HELL. **

THINK CAREFULLY & ACT WISELY...! MARRIAGE IS YOUR DESTINY..! 

MWL JOHN C NTOGWISANGU

WATSAP 0712463344

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.