Mwl Ntogwisangu JC.
Kuna maeneo kama 5 tutaenda kujifunza Katika mfululizo wa somo hili, Leo tunaenda kuangalia sehemu ya kwanza yenye kichwa kinachosema 👇
▫NINI MAANA YA KUWA KICHWA KWA MKEO /FAMILIA...!
🔹Maandiko yanaweka wazi ukweli kuwa mwanaume ni KICHWA kwa mkewe na familia kwa ujumla.
"Kwa maana Mume ni KICHWA cha mkewe, kama Kristo (YESU) naye ni kichwa cha kanisa, naye ni mwokozi wa Mwili "
Warumi 5 :23
🔹Biblia inaposema mwanaume ni kichwa ina maana kuwa mwanaume ndiye kiongozi, mtu anayetakiwa kubeba Maono, kuiongoza na kufanya Maamuzi Kwa mkewe na familia.
🔹Hii ina maanisha mwanamke anapaswa kusikiliza na kutii maongozi ya mume wake, pale panapokuwa na tatizo basi mwanaume anapaswa kutoa majibu ya matatizo hayo.
🔹Mwanamke anapaswa kumsikiliza na kumtii mumewe Katika YOTE, msisitizo upo kwenye hilo neno YOTE KAMA vile kanisa linavyomtii Kristo Katika YOTE.
🔹Lakini Je mwanaume hakosei? Mwanaume anafahamu kila kitu? Mwanamke hawezi kutoa muelekeo wa familia? La hasha..! Hii si maana ya kuwa kichwa.
🔹Mwanaume ingawa yeye ni kichwa lakini si mara ZOTE Atakuwa sahihi, atakuwa anajua kila kitu, si mara zote atakuwa na majibu kamili, kama ni hivyo basi asingehitaji kuwa na mwenzake maana amekamilika kwa kila kitu.
🔹Mungu alimpa Adam MSAIDIZI na si mke (Mwanzo 2 :18). Neno msaidizi limetumika hapa badala ya mke ili kuleta lengo kuu la Mungu la kumleta Hawa kwa Adamu.
🔹Mungu alimtaka Hawa awe msaidizi, msaidizi wa nini? Msaidizi wa kutimiza MAONO aliyompa Adamu, na jukumu mojawapo la Hawa Katika kutimiza usaidizi wake ni KUMSHAURI Adamu.
🔹Mwanamke ni mshauri mzuri sana pale anapopewa nafasi hiyo, ndio maana ibilisi alimtumia Hawa kumshalawishi Adamu kufanya dhambi. Cha kusikitisha baadhi ya wanaume wanawachukulia wanawake kama ni watu wa kupelekwa TU, pale wanaposhauriwa hupuuzia ushauri huo na hata wengine wanaona wakishauriwa kama wamedharauliwa.
🔹Aisee, huu mtazamo si sahihi hata kidogo, wanaume wengi wameshindwa kufanikiwa Katika maisha yao kwa sababu ya kutowashirikisha au kusikiliza wenzi wao, hata familia zingine hazipigi hatua kimaisha kutokana na kutokuwapa nafasi wake zao.
🔹Kama haumini ushauri wa mwanamke wako kwanin ulitaka kuwa nae? Ulimuoa ili iweje? Akuzalie watoto? Akufulie Nguo zako na kukupikia? Mbona hata madobi na mamantilie wapo..! Ulimuoa ili akutimizie haja zako za Mwili? Kama ni hivyo kuna Utofauti gani kati ya binadamu na wanayama, maana hata wao hutimiziana haja za miili yao.
🔹Mahusiano mazuri na NDOA yenye Baraka ni ile amabayo wahusika hushauriana na kupanga mambo kwa pamoja. Biblia inasema 👇
"AFADHALI KUWA WAWILI KULIKO MMOJA, MAANA WAPATA IJARA NJEMA KWA KAZI YAO "
MHUBIRI 4: 9
🔹Kuwa wawili hapo haimaanishi kulala chumba au kitanda kimoja, mnaweza mkalala wote lakini msiwe wawili. Haujawahi kusikia watu wapo kwenye ndoa lakini mwanaume hajui mshahara wa mkewe na mwanamke hajui mshahara wa mumewe na kila mtu ana Akaunti yake ya benki. Hawa kila mtu yupo peke yake.
🔹Hivyo kama mwanaume unatakiwa kufahamu kuwa ingawa wewe ndio kichwa lakini si kwamba unafahamu kila kitu na upo sahihi kwa kila kitu.
🔹Kubali kushauriwa, kubali kusema hapa sijui naomba msaada, kubali kukosolewa pale unapokesea. Acha mfumo dume, kukubali kushauriwa au kukosolewa hakukuvui Suruali yako na kufanya uonekane umevaa Sketi, zaidi itaongeza HESHIMA YAKO na kukufanya uwe mume Mwema na baba bora wa familia yako.
🔹MKE MZURI NI YULE MWENYE UJASIRI WA KUKUKOSOA, KUKUSHAURI NA KUKUREKEBISHA KWA HEKIMA PALE UNAPOKOSEA, NA SI MWANAMKE WA KILA KITU YEYE NI NDIO MZEE, HUU SI UTII BALI NI UOGA NA MZIGO KWAKO.
BE A GOOD HUSBAND & FATHER TO YOUR WIFE & FAMILY.
"NDANI YA KILA MWANAUME ALIYEFANIKIWA KUNA YESU, NA NYUMA YA KILA MWANAUME ALIYEFANIKIWA KUNA MWANAMKE MWENYE HEKIMA NA ANAYEJITAMBUA "
............... **.................... **........
MWL JOHN CHARLES NTOGWISANGU
KUJIUNGA NA MAGROUP YA NENO LA MUNGU WATSAP #0712463344
0 comments:
Post a Comment