Mwl Ntogwisangu JC
🔹Kuna watu wamekuwa waangaliaji wakubwa wa porn, na imefika mahali wameshindwa kujitoa kutokuangalia picha hizo na wengine wanauliza Je kuangalia picha za UCHI ni dhambi?
🔹Nitaenda kuelezea kwanin uangaliaji wa picha hizo ni dhambi na namna ya kujitoa Kuangalia picha hizo..
👉KWANINI NI DHAMBI..?
1. WANAOIGIZA SI WATU WANAOMJUA MUNGU.
🔹Picha hizo za uchi, zimetungwa na kuigizwa na watu wasiomjua Mungu, hivyo ubunifu na mafunzo hayo hayatokani na Mungu bali Katika hekima ya ulimwengu.
🔹Na jambo lolote lisilobeba hekima ya Mungu basi limebeba hekima ya Shetani, kama halijabeba kusudi la Mungu basi limebeba kusudi la Shetani, kama si la HAKI basi ni dhambi.
🔹Hakuna jibu la katikati, hivyo kwa wanaongalia picha hizo wanapokea hekima na mafundisho ya kishetani na wanakuwa Chini ya utawala wa kipepo.
2. HUAMSHA TAMAA YA NGONO.
🔹Picha hizo huchochea tamaa /hamasa ya kufanya tendo hilo, hivyo wengi Baada ya kuangalia picha hizo hujisikia hamu ya kufanya ngono au kufanya masturbation (kujichua).
🔹Yeye aliyeangalia porn, yule aliyefanya masturbation na aliyefanya ngono na mtu wote wanahesabika kuwa na DHAMBI.
"Lakin mimi Nawaambia, kila Mtu Amtazamaye mwanamke kwa Kumtamani AMEKWISHA KUZINI NAYE moyoni mwake " Mathayo 5 :28
🔹Je kama nimeoa kuangalia picha hizo ni dhambi? Hata kwa wanandoa bado picha hizo ni dhambi, kwa sababu unapoangalia picha hizo Mwili wako unasisimka na kuwaka tamaa ya mapenzi kwa kumuangalia mwanaume /mwanamke anayeigiza mkanda huo na si mkeo au mumeo, hivyo kwa kuatamani huko unakuwa umezini na mtu huyo na si mkeo /mumeo.
3. HUFUNDISHA SEX CHAFU.
🔹Mikanda mingi ya porn hufundisha njia za ufanyaji wa mapenzi ambazo ni kinyume na mapenzi ya Mungu. Mfano oral sex (kufanya mapenzi kupitia mdomo), anal sex (mapenzi kupitia njia ya haja kubwa) nk.
🔹Mungu alimuumba mwanaume na mwanamke na akakipa kila kiungo Katika Mwili Kazi yake maalum, hivyo kubadilisha Kazi ya viungo hivyo sio UBUNIFU bali ni UDANGANYIFU unaofanywa na Ibilisi na ni DHAMBI mbele za Mungu.
"Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za AIBU, hata wanawake Wakabadili MATUMIZI YA ASILI kwa MATUMIZI YASIYO YA ASILI " Warumi 1 :26.
4. HUCHOCHEA UZINZI KWENYE NDOA.
🔹Hapa nitaongelea kwa walio kwenye ndoa, Mikanda ya picha za uchi huchochea uzinzi kwenye ndoa, unaweza ukauliza kivipi..?
🔹Unapoangalia picha hizo unawaona watu wenye maumbile mbalimbali wenye matiti makubwa, wenye makalio makubwa, weupe, weusi, wanene, wembamba nk,
🔹Hivyo unaweza ukajikuta unaangalia mwanamke mwenye makalio makubwa kwenye huo mkanda au CD wakati mkeo ana umbo la ki 'mis (mwembamba) na wewe kwa kuangalia picha hizo unaweza ukajikuta ukatamani kumpata mwanamke na wewe mnene mwenye makalio makubwa (wowowo) ili ujaribu radha yake
🔹AU mwanamke , mume wako anaweza akawa na uume mdogo na hao unaowaangalia wakawa wana uume mkubwa hivyo ukatamani na wewe kumpata mwanaume kama huyo unayemuangalia kwa kuhisi utapata raha zaidi.
🔹Pia namna ambavyo mwanaume /mwanamke mwenzako anavyofanyiwa kwenye huo mkanda unaweza ukatamani na wewe mwenzi wako akufanyie, na kwa bahati mbaya akawa hawezi kufanya hivyo, Hii inaweza ikakuletea shida na kutamani labda uchepuke ili umpate mtu atakayekidhi matamanio yako.
👉NJIA ZA KUJITOA KUANGALIA PORN.
1 . FAHAMU KUWA NI DHAMBI
🔹Ni muhimu kufahamu kuwa uangaliaji wa porn ni dhambi na nini madhara yake.
2. DHAMIRIA KUACHA.
🔹Baada ya kufahamu kuwa ni machukizo mbele za Mungu kuangalia porn na kujua madhara yake, basi weka msimamo wa DHATI moyoni mwako wa kutoangalia TENA.
3. FUTA PICHA HIZO ZOTE.
🔹Huwezi kusema unataka kuacha kuangalia porn wakati simu, laptop yako na chumbani kwako umejaza ma CD ya picha hizo.
🔹Futa /haribu na Ondoa mikanda /CD zote za Porn kwenye simu, laptop na sehemu yoyote ulipozihifadhi, Ili usije ukapata kishawishi cha kuangalia tena.
"Jicho lako la kuume likikukosesha, LING'OE ULITUPE MBALI nawe, kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala Mwili wako mzima usitupwe Katika JEHANUM "
Mathayo 5 :29
4. JITENGE NA MARAFIKI WABAYA.
🔹Rafiki wa mtumishi ni mtumishi, rafiki wa mzinzi ni mzinzi na rafiki wa mwangalia Porn ni muangalia Porn.
" Chuma hunoa Chuma, Ndivyo mtu aunoavyo Uso wa Rafiki yake "
Mithali 27 :17
" Birds of the same feathers fly together "
5. AMUA KUMTAFUTA MUNGU.
🔹Unapoangalia picha za porn unakuwa kwenye kifungo kamili cha MAPEPO, ndio maana wakati mwingine unaweza kutamani kuacha lakini unakuta kuna msukumo usio wa kawaida unaokulazimisha uendelee kuangalia.
🔹Sasa ili uweze kutoka kwenye kifungo hicho unatakiwa uingie kwenye Maombi ya TOBA (Zaburi 51).
"Basi Mtiini Mungu, MPINGENI SHETANI naye ATAWAKIMBIA "
Yakobo 4 : 7
🔹Na wakati mwingine utahitajika kufanya Maombi ya KUFUNGA pia ili UFUNGULIWE.
" Lakini namna Hii HAITOKI ila kwa KUSALI NA KUFUNGA "
Mathayo 17 : 21
MWISHO : OMBA MUNGU AKUPE NGUVU YA KUISHI MAISHA YA UTAKATIFU, TAMANI KUWA NA USHIRIKA NA ROHO MTAKATIFU PIA JITOE KUMTUMIKIA MUNGU.
" MTAKUWA WATAKATIFU KAMA MIMI (MUNGU) NILIVYO MTAKATIFU "
1 PETRO 1 : 16
......................... END................
MWL JOHN C NTOGWISANGU
MAOMBI, USHAURI NA MAFUNDISHO
👉KUJIUNGA NA KANISA LA WATSAP #0712463344
Amen!!!!
ReplyDelete