Entertainment


KUJIANDAA KUWA MUME BORA

KUWA KIOO KWA MKEO..!

Mwl Ntogwisangu JC. Watsap (0712463344)

Leo tunaendelea na sehemu ya PILI ya somo letu la namna ya kujiandaa kuwa mume na baba bora wa familia.

🔹Mwanamke asili yake ni kujiremba na kutaka kuonekana mzuri na mwenye mvuto Katika jamii na hasa mbele ya mwanaume.

🔹Hutumia muda mwingi sana kujiremba na kukaa kwenye Kioo. Hubadilisha mitindo ya nywele karibu kila wiki, mara Leo kaweka wigi kesho kasuka yeboyebo sijui zile za mmasai ili mradi tu aonekane kapendeza na mwenye mvuto machon pa watu.

🔹Wakati mwingine atanyoa nyusi na kujichora na penseli yaani Mwili unakuwa kama daftari, wenyewe huwa wanaita wanja, atapaka marangi mdomoni, kwenye kucha, kope bila kusahau ule unga mweupe wanaopaka usoni unajulikana pia kwa jina la poda.

🔹Yote haya ni ili tu ajisikie kuwa ni wa thamani machoni pa watu. Ndio maana wengine humuita mwanamke ni pambo, unajiuliza pambo la nini? Ni pambo la Mwanaume.

🔹Sasa hapa ndipo nataka wanaume waelewe kitu, vurugu zoote hizo za kujikwatua anazofanya ni kwa ajili yako, ndio ni kwa ajili yako na si mtu mwingine.

🔹Ndio maana wanawake wengi Baada ya kuolewa zile mbwembwe za kujikwatua huwa zinapungua kama sio kuisha na wanabaki wa kawaida, sasa kama ulidanganywa na poda hapo Kazi unayo.

🔹Na huwa najiuliza kama wanawake wangekuwa peke yako, hivi hizi vurugu za kushindana mitindo hivi zingekuwepo kweli? Sijui, lakin sidhani kama zingekuwepo. Na hata kama zingekuwepo isingekuwa kwa kiasi hiki.

🔹Sasa kama mwanaume ni vizuri ufahamu hili, unapoona anatumia pesa nyingi kujiremba na kununua vitu visivyo na ulazima sana, usiwe na hasira ukaanza kumfokea na kumwona hafai. La hasha..! Hiyo ndio asili yake.

🔹Unachotakiwa kufanya ni kufahamu psychology yao na kuenda naye polepole, Biblia inasema tukae nao kwa akili (1 Petro 3 :7). Sasa naomba nikupe kidogo hiyo akili ya kuchukuliana nao.

🔹Hapa unatakiwa kucheza na AKILI yake na kuanza kumsifia kila anapotaka kutoka au anapobadili mtindo mpya wa nywele, we mwambie "waaoh, umependeza sana mke wangu", "you look so beautiful my dear "na maneno mazuri kama haya.

🔹Na kama siku amesuka nywele zile za kawaida au amevaa simple sana, hapo sasa ndio unakoleza sifa mpaka basi," yaaan mke wangu aisee ulivyopendeza Leo sijawahi ona yaaan acha tu" anaweza asikuamini akaona kama unamtania lakini wewe koleza zaidi sifa na kuonesha msisitizo siku hiyo mtoe 'OUT' mkanywe hata Soda.

🔹Unaweza usielewe kwanin nakuambia ufanye hivi. Subir nikuambie psychology nyingine ya mwanamke ni kupenda sana KUSIFIWA yaani hata kama hajala kitu anaweza kujiona ameshiba.

🔹Unapomsifia unajenga hali ya KUJIAMINI ndani yake na kujiona kuwa ni mzuri, pale anapohisi ajapendeza muambie umependeza sana, hii itamfanya aanze kujikubali, kujipenda na kujiona wa thamani.

🔹Wanawake ambao wanajiremba kupita kiasi wengi wao husumbuliwa na kuwa na 'Low self esteem' nikimaanisha hali ya kutokujikubali na kujiamini. Na dawa ya ugonjwa huu ni KUMSIFIA TU wala hahitaji Panadol wala kukemea Pepo.

🔹Nimekuibia Siri hii, ebu itumie na uone mabadiliko. Anza kumsifia kila siku anapotaka kutoka, anapobadili mitindo yake ya nywele au Nguo, akiwa anajiangalia kwenye Kioo basi kaa mbele yake msaidie kumtengeneza vizuri na mwambie 'Nakupenda sana mke wangu mzuri', 'umependeza sana' , 'Nashukuru Mungu kunipatia mrembo kama wewe' .

🔹Hivi ndivyo Mwanaume anapaswa kumfanyia mke wake, na si kumkaripia na kumtolea maneno mabaya, eti kisa anatumia pesa nyingi kujiremba,au kwa sababu anakuchelewesha kila mnapotaka kutoka.

🔹Jenga utamaduni wa kumsifia, amfanye ajiamini na ajione ni wa thamani, Usiruhusu aanglie Kioo anapojiandaa, ebu fanya wewe ndio Kioo chake kwa kumuandaa kisha mwambie kuwa Umependeza.

🔹Yale Masaa ya kukaa kwenye Kioo yatapungua na hali ya kujiremba kama kinyago pia ITAKOMA.. Hii ndiyo TIBA YA ASILI isiyohitaji mzizi wowote zaidi ya nyama ya ulimi (maneno matamu).

🔹Imeandikwa.... "ENYI WAUME WAPENDENI WAKE ZENU, KAMA KRISTO ALIVYOLIPENDA KANISA AKAJITOA KWA AJILI YAKE"

"VIVYO HIVYO IMEWAPASA WAUME NAO KUWAPENDA WAKE ZAO KAMA MIILI YAO WENYEWE "

                      WAEFESO 5 :25, 28

🔹Naomba niishie hapa kwa Leo, tutaendelea wakati mwingine.. 👋👋

BE GENTLY TO YOUR WIFE & TREAT HER PATIENTLY, SINCE SHE IS YOUR BODY AND SOUL.

MWL JOHN CHARLES NTOGWISANGU

👉KUJIUNGA NA MAGROUP YA WATSAP 0625063205, 071300654
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.