KWANINI VIJANA WALIOOKOKA HUONA NA WATU WA MATAIFA
KWANINI VIJANA WALIOOKOKA HUJIINGIZA KWENYE MAHUSIANO NA WATU WA MATAIFA..!
🔹Zipo sababu kadhaa zinazopelekea Vijana wengi waliokoka sasa kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na watu wasiookoka na hata baadhi yao kuoa /kuolewa nao.
🔹Zifuatazo ni sababu hizo 👇
👉KUTOTAMBUA THAMAN YAO.
🔹Vijana wengi sasa hawaelewi thamani yao, hawaelewi kuwa wao ni uzao mteule. Na wengi Leo hata hawaelewi nini maana ya wokovu, hawana hata maandiko yanayosimamia Imani yao, hawana ujasir wa Kukiri kama wameokoka,kwa ufupi hawajitambui.
🔹Kama ukishindwa kujitambulisha kwa watu kuwa umeokoka na kama maisha yako hayana ushuhuda kama wewe ni mteule yaan mtu anapokuangalia wewe na vijana wengine hapo kazini, shuleni, chuoni au sehemu unayoishi na haoni utofauti basi ujue hapo kuna shida, ni lazima uingie kwenye mtego wa Shetani.
👉KUTUMIA VIBAYA NEEMA /UHURU WALIO NAO KATIKA KRISTO.
🔹Ndani ya wokovu hatuiishi kwa sheria, hatutumii sheria ili kujilinda na dhambi lakini hii haimaanisha kuwa tuwe HURU kupita kiasi na kuishi bila mipaka ya Imani yetu.
"TUSEME NINI BASI? TUDUMU KATIKA DHAMBI ILI NEEMA IZIDI KUWA NYINGI? " WARUMI 6:1.
🔹Lakini Vijana wa sasa wanaishi kiholela bila UTARATIBU, kuhusu swala la kuoa /kuolewa maandiko yanaeleza wazi kabisa kuwa hatutakiwi kuoana na watu wasiomjua Mungu 👇
" MSIFUNGIWE NIRA (MSIOANE) PAMOJA NA WATU WASIOAMINI (WASIOOKOKA), KWA JINSI ISIVYO SAWASAWA, KWA MAANA PANA URAFIKI GANI KATI YA HAKI NA UASI, TENA PANA SHIRIKA GANI KATI YA NURU NA GIZA? "
2 WAKORINTHO 6 :14
SOMA PIA :MATHAYO 6 :1-5, KUMBUKUMBU 7 :2 - 4.
🔹Lakin jambo la kushangaza Vijana wa sasa wanakiuka utaratibu huo na Agizo hilo kwa makusudi, na Kusema eti atambadilisha mbele ya safari. Hivi kama ameshindwa kubadilika sasa ndio atabadilika baadaye? Kuna msemo usemao samaki mkunje angali Mbichi.
🔹Kuwa na mtu asiyeookoka na Kusema kama utambadilisha ni sawa na DHAMBI YA KUMJARIBU MUNGU maana unafahamu ukweli lakin unaupinga kwa tamaa zako binafsi, kufanya hivyo ni sawa na KUMDHIHAKI MUNGU lakini Neno linasema Mungu HADHIHAKIWI maana chochote apandacho mtu ndicho ATAKACHOVUNA (GALATIA 6 :7).
👉UTANDAWAZI
🔹Kuongezeka kwa utandawazi kumechangia pia kwa kiasi kikubwa kuanguka kwa Vijana wengi Kiroho. Maisha ya kuiga tamaduni za wageni yameharibu Vijana wengi nje na Ndani ya kanisa.
🔹Muingiliano wa watu umekuwa mkubwa sana na Muingiliano huu unajaribu kuwafanya watu wafanane Katika namna ya maisha, hapo wateule ndipo tunajisahau na kuchangamana na mataifa wakati NENO linasema TUSIIFUATISHE NAMNA YA DUNIA. YAKOBO 4 :4
🔹Kuna tofaut kubwa sana kati yetu na wao, ingawa ni rafik zetu na jamaa zetu lakini damu ya YESU imetutenga na kutufanya tuwe tofaut nao. KOLOSAI 1 :13
👉TAMAA YA KUOA /KUOLEWA.
🔹Msukumo wa kuoa /kuolewa kwa Vijana wengi wa sasa huwafanya kuingia kwenye mahusiano mabovu yasiyo na utaratibu wa KIMUNGU.
🔹Msukumo huu huwa ni mkubwa sana kwa mabinti kuliko Vijana wa kiume, na kujikuta wakiwa Katika mtego wa muwindaji (Ibilisi).
🔹Kila jambo lina wakati wake, Ni HERI Uchelewe kufika kuliko kuwahi KUJUTA.
👉VITA YA KIROHO
🔹Ibilisi anajua kuwa ni Nguvu kazi ya kanisa hivyo lazima apige vita sana hapo na awaingize kwenye ndoa mbovu. Maana kila kitu kizur au kibaya kinaanzia kwenye ndoa /familia.
🔹Ndani ya familia ndio panapatikana wahubiri, wachungaji, waalimu, viongozi wa nchi na watu wenye nyazifa mbalimbali lakini ndani ya familia hiyo tunaweza kupata majambazi, makahaba, wachawi nk.
🔹Na kanisa ili liweze KUENDELEA linahitaji Vijana wanaomjua Mungu na waliojazwa Roho Mtakatifu na vijana hao lazima watoke kwenye familia fulani, hivyo kama familia ni mbovu hata HUDUMA pia itakuwa mbovu haitapata KIBALI.
🔹Na ndio maana Ibilisi anapiga vita sana Vijana wasiifikie Ndoa Salama iliyo na UTUKUFU wa Mungu.
.............
👉KIJANA, SIMAMA KATIKA NAFASI YAKO, USIKUBALI KUMUACHA MUNGU KWA AJILI YA MTU AU KITU CHOCHOTE. WARUMI 8 :35
👇▫CHOCHOTE KINAWEZA KUKUACHA WAKATI WOWOTE, LAKINI YESU ATAKUWA NAWE, WAKATI WOTE KATIKA YOTE. ▫SHINDA TAMAA YA MOYO.
YEREMIA 17:9
0 comments:
Post a Comment