Entertainment


MWANAMKE JIVIKE KIREMBA CHA HEKIMA NA UTII



MWANAMKE JIVIKE KIREMBA CHA UTII NA HEKIMA..! 

Ndoa nyingi na mahusiano mengi yamevunjika kutokana na wanawake wengi wa sasa kushindwa kutambua NAFASI zao. Sitofahamu zimekuwa nyingi sana katika mahusiano ya sasa, kiukweli yanakatisha tamaa, yanavunja moyo. Shida ipo wapi?

Wanawake wengi wa sasa wameshindwa kuelewa ni wapi pa kuongea na ni wapi pa kukaa kimya, si kila wakati ni wa kusema (kuna kipindi ukimya wako una maana zaidi ya maneno 1000 unayoweza kuongea) na hata kama unaongea si kila sehemu ni ya kuongea (yapo mazingira sahihi ya kuongelea ya kila jambo) vile vile hata kama ni wakat sahihi na mazingira sahihi ya kusema, kuna namna pia ya kusema /kuwasilisha jambo lako (si kila maneno yanafaa kubeba wazo au hisia zako). Hapa kuna changamoto kubwa sana kwa wanawake wengi na ni chanzo pia cha migogoro mingi isiyo na ulazima kwenye chumba au ndoa.

Uwezo wa kujua wapi pa kuongea, sehemu gani ya kuongea na jinsi gani ya kuongea kwa neno moja huitwa HEKIMA, ambayo ni ya umuhimu zaid kwa mwanamke kuliko sura, umbile au mapambambo mbalimbali unayoweza kutumia mwanamke. Ni hekima pekee isiyozeeka wala kupoteza uzuri wake, mwili, shape na mapambo yote unayotumia vina tabia ya kufifia na kupoteza uzuri wake wa asili.

"Ni nani aliye kama mwenye HEKIMA, naye ni nani ajuaye kufasiri neno? HEKIMA YA MTU HUMNG'ARIZA USO WAKE NA UGUMU WA USO WAKE HUBADILIKA "
       
                      MHUBIRI 8 :1.

Tena mwanamke mzuri aliyekosa HEKIMA hana THAMANI mbele za Mungu na mwanaume, biblia humlinganisha hivi :

" Kama PETE YA DHAHABU puani mwa NGURUWE, kadhalika MWANAMKE MZURI ASIYE NA AKILI "

                       MITHALI 11 :22

Cha kusikitisha wanawake wengi wa sasa mmekosa sifa hii, na bila kujua mnajikuta mnachumbiwa na kuachwa au kwa walioolewa ndoa kuvunjika, badala ya kubaki ukilalamika kuwa wanaume hawafai si wa kweli, Ebu JICHUNGUZE kama una sifa ya HEKIMA na UTII ndani yako, isikute kati ya wanaume uliokuwa nao wapo walikuwa wanahitaji kukuoa lakini badala ya kuona KIBURI, DHARAU na KUTOKUBALI KUSHUKA waliamua kubadilisha mawazo.

 Hivi ni nani anayependa kuukumbatia MOTO? TABIA ZA WANAWAKE WENGINE NI KAMA MOTO.!

Sifa ya mwanamke nyingine ni UTII na USIKIVU ambayo zinaenda sambamba na HEKIMA, mwanamke anapaswa kuwa chini na kukubali KUONGOZWA na mwanaume, anapaswa kumsikiliza na kumtii mwanaume. Hivi ndivyo hata Mungu ameagiza,

"Enyi wake WATIINI WAUME ZENU kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni KICHWA cha MKEWE, Kama kristo naye ni KICHWA cha kanisa, naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo WAKE nao WAWATII WAUME ZAO KATIKA KILA JAMBO "

              WAEFESO 5 :22-24.

Mwanaume ndio KICHWA (kiongozi) wa mwanamke na ndiye anapaswa kutoa muelekeo wa mambo mbalimbali katika uhusiano (uchumba au ndoa) na mwanamke anapaswa kusikiliza na kufuata maelekezo hayo, na mwanaume yeye ameagizwa KUMPENDA na si KUMTII mke wake. Wakolosai 3 :19..! Hivyo mwanamke amewekewa UTII wakat mwanaume ameagizwa UPENDO kwa mke wake (HIVI VINAPASWA KUENDA SAWA KILA UPANDE).

Na hata katika kuumbwa mwanaume aliumbwa kwanza ndipo mwanamke akafuata baadaye. Mwanzo 2 :21-22.Kwa bahati mbaya tunapokuwa tunasema wanawake wanapaswa kuwatii wanaume, wanawake wengi wanaona kama vile WANAKANDAMIZWA Na KUONEWA na kwa udanganyifu wa IBILISI aliwatia watu upumbavu wa kuazisha DHAMBI YA KUKIUKA UUMBAJI WA MUNGU kwa jina la HAKI ZA WANAWAKE (WOMAN EMPOWERMENT) na wakaja na kauli mbiu ya kusema HAKI SAWA KWA WOTE. Hii imewatia ujinga wasichana wengi na kuwafanya wakose kuona raha ya kuwa wanawake.

Tena kwa bahati mbaya binti atokee kuwa amesoma au ana uwezo kumzidi mwanaume hapo ndipo utakapoona HAKI SAWA inavyofanya Kazi yake. Wanawake hawa hawakubali kushuka, hawakubali KUONGOZWA na mwanaume wanataka kujiongoza wenyewe. Wanajiona ni wanawake wa kisasa 'modern women' Wanajiona kuwa wameelimika lakini kiukweli wamelaanika na si kuelimika. Wamepoteza sifa ya uanamke wamekuwa sasa na JINSIA MBILI. (uanamke na uanaume).

Unaweza ukaona binti amevaa suruali ukafikiri ni FASHION TU Lakini ukichunguza wengi wao vazi hilo la suruali limeathiri mpaka FIKRA ZAO, wanawaza kama wanaume, wanapenda kushindana na wanaume, hawataki KUONGOZWA na wanaume. FIKRA ZAO ZIMEVAA SURUALI. Ni wanawake kwa nje ila ndani ni wanaume.

Utakuta binti kajiremba mwenyewe kapendeza, kama ukiniuliza namuaonaje nitakuambia "she is looking handsome" na si "she is looking beautiful" kwa sababu ni kweli kapendeza kwa nje kama msichana kwa mavaz yake lakini ndani yake ana mawazo ya kutaka kujiongoza (mawazo ya kiuanaume) hvyo sio beautiful tena bali ni handsome. U beautiful si mavaz tu bali pia na mind (ufahamu), Je tabia yako inavutia wanaume wa kuoa? Au mavaz yako yanavutia wanaume wa kulala na wewe tu kama kiburudisho na KUKUACHA?

 Kama una FIKRA za kiume unataka mwanaume wa nini? Ni mwanaume gani anataka kuoa mwanaume mwezake (jike dume)? Sijui labda wapo, subir watakaozaliwa ila kwa hawa waliopo sasa SAHAU DADA YANGU.

Utakuta Dada mzuri ana Kazi yake miaka zaidi ya 30 hana mume ila ana watoto 3 au 4 na kila mtoto ana baba yake, wa kwanza alizaa na mhasibu, wa pili alizaa na daktar na watatu amezaa na manager wa bank fulani. Dada shida ipo wapi? Kwanini wanaume wote hao wasikuoe? Ni wanaume wenye shida au wewe ndiye mwenye shida? JICHUNGUZE. Sikiliza hata kama una Kazi nzuri na maisha yanaenda kama huna mume HESHIMA yako inashuka kwenye jamii na kuonekana MUHUNI kama walivyo wahuni wengine ila wewe ni muhuni uliyesoma.

Ninaposema umtii mwanaume haina maana kuwa mwanaume yeye yupo sahihi kwenye kila jambo au anajua kila kitu kuliko wewe, inawezekana ukawa na mawazo MAZURI kabisa yanayofaa shida unayafikishaje mawazo hayo? Je umetengeneza mazingira ya ushawishi? Umetumia lugha gani kuyafikisha mawazo hayo? Shida ipo hapo. Shida si WAZO lako shida ni wewe unayeliwasilisha WAZO hilo. Kuna wanaume ambao ni rahis kushaurika na wapo ambao ni wagumu kushaurika (watu tumetofautiana) sasa inabidi umsome mwanaume wako ni mtu wa namna gani.

Kama ana tabia ya ubishi kushaurika usitumie NGUVU ya maneno makali, kumtuhumu vibaya au kugoma na kuonesha KIBURI kufanya hivyo hakutatui tatizo bali huchochea tatizo. Tafuta mazingira mazur, wakati mzuri akiwa ametulia, fanya kitu kizuri ambacho huwa anapenda (nadhan unakijua) kisha ingiza jambo lako hapo uone kama ATAKATAA TENA
.
Biblia inamuelezea mwanamke mmoja aliyeitwa Esther ambaye kwa kutumia Nguvu yake ya HEKIMA NA USHAWISHI aliyompa Mungu aliweza kuwaokoa Waisraeli wote ambao walitakiwa kuuwawa. Soma kitabu cha Esta sura ya 8. kwa kutumia HEKIMA yako unaweza ukaiponya ndoa yako na nyumba yako, na kwa upumbavu wako unaweza ukaharibu ndoa yako na familia yako pia.

"Kila mwanamke aliye na HEKIMA HUJENGA nyumba yake, Bali aliye mpumbavu HUIBOMOA kwa mikono yake mwenyewe. " Mithali 14 :1

Ndoa za wazee wetu zilidumu si kwasababu walikuwa hawagombani, au kulikuwa hakuna michepuko bali wanawake (mama zetu na bibi zetu) walikuwa wavumilivu na walitambua nafas zao tofaut na wasichana wengi wa sasa, na si kwamba wanaume (baba na babu zetu) walikuwa wastaarabu na waaminifu sana kuliko wanaume wa sasa. Ndoa kusimama au kuvunjika kunategemea sana na mwanamke yupoje na si mwanaume yupoje. MWANAMKE NDIO MUHIMILI WA NYUMBA MWANAUME NI KIONGOZI TU.

Mwanaume akikosea haina haja ya kumlazimisha akiri kosa hilo kwa wakati huo (tafuta muda mwingine muambie kwa upole atakuelewa), akipanda juu wewe shuka chini (kujishusha si ujinga, ni hekima na sifa ya mwanamke). Dawa ya moto si MOTO.

Mwanamke Mungu amekuumbia nguvu kubwa sana ya USHAWISHI kwa mwanaume kama UKIJITAMBUA NA KUITUMIA NGUVU HIYO YA ASILI. hakuna mwanaume aliye mjanja au hodari kwa mwanamke mwenye USHAWISHI NA HEKIMA hata awe shujaa wa namna gan ATAKUWA kama mtoto mdogo wa kubebwa mgongoni.

 WANAWAKE MNAWEZA MKIJITAMBUA.

ACHA MAMBO YA HAKI SAWA, ACHA FIKRA ZA KIUME ZA KUTAKA KUJIONGOZA, JIVIKE KIREMBA CHA HEKIMA NA UTII, JIVUNIE KUWA MWANAMKE, ISHI KAMA MWANAMKE. FURAHIA KUWA MWANAMKE.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.