ACHA MAISHA YAENDELEE
ACHA MAISHA YAENDELEE...!!
Haina haja ya kuumia kwa ajili ya mtu asiyetambua thaman yako kwake.. Yupo mwingine atakayekuthamini.. …..Acha maisha yaendelee..!
Haina haja kumchukia mtu asiyekupenda.. Kukupenda au kutokukupenda ni hiari yake. ………..Acha maisha yaendelee..!
Haina haja ya kumuwekea kisasi mtu asiyekupenda au aliyekuacha. Kumbuka hakuna adhabu kwake kwa kushindwa kukupenda au kusitisha mahusiano na wewe………… Acha maisha yaendelee..!
Haina haja ya kumsema vibaya kwa watu na kubeba chuki dhidi yake. Kumbuka hasira na wivu ni viashiria vya ugonjwa wa kuwa na 'low self esteem' yaan mtu asiyejikubali au kujiamini, mtu anayejiamini huumia, hujikaza na kuendelea mbele. Kama uliweza kuwa na yeye kwanin ushindwe kuwa na mwingine?Jiamini……Acha maisha yaendelee..!
Haina haja ya kukata tamaa na kufurahia maisha yako eti kwa sababu fulani amekuacha. Mwache aende, alikuja kwa hiari yake na ameamua kuondoka kwa hiari yake……….. Acha maisha yaendelee..!
MWISHO : kumbuka maisha yako na furaha yako haipo mikononi mwa mtu yeyote yule, isipokuwa wewe mwenyewe. Tafakari ni wapi ulikosea, chukua hatua ya kuanza maisha mpya. Binadamu tunajifunza kutokana na makosa.
ACHA MAISHA YAENDELEE...!!
0 comments:
Post a Comment