UNA SIFA YA KUWA MKE?
ARE YOU WIFE MATERIAL ? (una sifa za kuwa mke?)
Ni kwa muda mrefu umelia kutokana na kuumizwa na wanaume, umekuwa na majeraha mengi na vidonda visivyo tibika hadi umefikia hatua ya kuona mapenzi machungu na kutamani kuishi peke yako, pengine umefikia mahali unaona bora utafute mtu wa kuzaa nae tu ila si kuolewa.
'wanaume ni waongo ',' wanaume wote ni wale wale '., mapenzi ya siku hizi hayana maana' 'bora niishi peke yangu ' Ni kauli ambazo mara nyingi unajiambia.. Lakin labda nikuulize ulishawahi kujiuliza kwanin hayo yote yanakupata? Ulishawah kujiuliza tatizo lipo wapi? Kujua tatizo ni nusu ya kupata suluhisho la tatizo.!
Nikusaidie sehemu ambayo wasichana wengi mnafeli, unajua jinsi unavyojiweka ndivyo watu watakavyokuchukulia, jinsi unavyo vaa, mambo unayo yawaza na jinsi unavyoongea utavuta aina ya marafiki na wanaume wanaofanana na wewe 'Equal attracts equal' psychology inasema hivyo, au kwa lugha nyingine watalaam wanaita 'law of attraction'.!
Eneo la kwanza la kuangalia, ni jinsi unavyo vaa..! Nguo unazo vaa zinakutambulishaje kwa watu? Nguo za kuacha maziwa yako yote nje, nguo zinakubana na kukuonesha maumbile yako yote mpaka nguo ya ndani uliyo vaa inaonekana, mapaja asilimia kubwa yapo nje.. Kwa uvaaji huu unategemea kupata mwanaume 'decent' wa kukuoa? Je unastahili kupelekwa ukweni na kutambulishwa kuwa ni mchumba na mke wa mtu mtarajiwa? Sikiliza ni kweli uvaaji huo utakufanya kuwavutia wanaume wengi lakini si wa kukuoa, hao wataishia kukusifia mzuri, kukutongoza, kulala na wewe kisha kukuacha.
Hakuna mwanaume anayependa mwanamke wa future anayevaa nguo zisizo na heshima, hata kama atakuambia anakupenda basi atakufanya uwe demu wa kupotezea muda tu na muda wa kuoa ukifika ataku'damp na kumchukua mwingine. Kumbuka 'hata mwizi hapendi kuibiwa'.
Acha kuishi maisha ya tamthilia, acha kujifafanya unaenda na wakati, wakati huwezi kushindana nao utaishia kujishushia heshima yako bure. Mavazi ni kitambulisho kikubwa sana, ukimuona askar utamfahamu kwa kuangalia nguo zake, ukimuona daktari utamfahamu kwa kuangalia nguo zake, mchungaji, shekhe, n. k Je nguo zako zinakutambulisha wewe nani? Kuwa mpole, acha wakati upite wewe baki na heshima yako.!
Jambo lingine la kuangalia ni jinsi unavyo waza na maongezi unayoongea.! Una miaka 2 au 3 upo kwenye uhusiano kila siku maongezi yako ni 'baby umeamkaje', 'umekula? ',' hubby nimekumic ',' leo utanitoa out? ',' kuna blauzi nzuri nimeiona utaninunulia? 'hivi hakuna maongez mengine ya maana ya kuongea mbali na hayo? Kama una umri chini ya 20 una haki kufanya hayo, lakini kama upo zaidi ya hapo dada yangu nakupa Pole.
Kama kijana uliye nae wewe ni msichana wake wa 3 au 4 ni kitu gani atakiona kwako cha utofaut ili umshawishi kukuoa akilinganisha na wale wasichana wake waliopita? Be creative dada! Ndoa si kitu Cha mchezo.
Kwanin usitake kujua ana mipango gani kwenye maisha? Kwanin usimshauri kununua kiwanja au kufungua biashara? Kwanin usimuambie mjaribu kupunguza out zisizo na lazima na muweke pesa bank? Utaniambia mambo hayo utayafanya kwenye ndoa ukiolewa, Nyota njema uonekana asubuhi kama sijayaona hayo sasa ya nini kufikiria kuwa na wewe? Jenga ushawishi mapema.!
Unatumia muda mwingi kubadilisha mitindo ya nguo na nywele, kila wigi unataka kununua. Hivi unafikir ukiwa kwenye ndoa tutakula wigi lako? Na hayo makucha uliyofuga utaweza kunifulia nguo kweli? Utaweza kufua nepi za watoto? Si utaniambia nitafute msichana wa Kazi au washing machine mikono itachubuka?
Sikiliza dada yangu nikuambie hakuna furaha kwa mwanaume kama kumuona mke wake akimfulia nguo, kunyosha nguo zake, kumpikia n. k hata kama si kila siku lakini atapenda akuone ukifmfanyia hayo pindi ukipata nafasi na si binti wa Kazi.
Unataka kuolewa na mwanaume mwenye pesa ili upate mtelemko, Sikiliza dada hakuna mwanaume anayependa goalkeeper hata kama ana uwezo, nowdays wanaume wanataka wanawake ma'fighter kwa lugha ya kisaa wanasema 'jembe'. Badilika, jirembe sawa lakini usisahau kuuremba uzuri wako wa ndani ambao ni UFAHAMU wako kama mwanamke.! Uzuri wako bila kuwa na akili nzuri biblia inafananisha na kitu Cha THAMANI kilicho sehemu ya OVYO isiyo na HESHIMA.
"mwanamke mzuri asiye na akili ni kama Pete ya DHAHABU puani mwa NGURUWE " Mithali 11:22..!
Hapa sijaongolea kuhusu lugha za mkato unazo mjibu mpenzi wako, kiburi, hasira na kununa bila sababu za msingi, kuruhusu mwanaume kulala na wewe kabla ya ndoa (NA HAPA KUNA SHIDA SI KIDOGO) muda haunitoshi kuyaongolea hayo kwa sasa, Mungu akipenda tutayaangalia siku nyingine. lakin kwanin mwanamke? Kwa sababu wewe ndio muhimili mkubwa wa ndoa, kusimama au kuvunjika kwa ndoa kuna kutegemea wewe. Ndoa itapona kwa HEKIMA yako na itavunjwa na UPUMBAVU wako.!
Naomba niishie hapa kwa leo...!
BE STRONG WOMAN, BE WOMAN OF PRINCIPLES, BE A GOOD WIFE, BE A ROLE MODEL TO YOUR CHILDREN.!
kumuelimisha mwanamke ni kuelimisha jamii, I HOPE NIMEELIMISHA JAMII.!
# WANAWAKE MNAWEZA MKIJITAMBUA #
0 comments:
Post a Comment